-
Mafuta Ni Muhimu Maishani MwakoAmkeni!—2003 | Novemba 8
-
-
Mafuta yalipata umaarufu yalipoanza kutumiwa kuwasha taa. Katika karne ya 15, mafuta yaliyotoka kwenye visima visivyo na kina kirefu yalitumiwa kuwasha taa huko Baku, jiji kuu la Azerbaijan. Katika mwaka wa 1650, visima vya mafuta visivyo na kina kirefu vilichimbwa huko Rumania, ambako mafuta yalitumiwa kuwasha taa. Kufikia katikati ya karne ya 19, biashara ya mafuta ilikuwa imesitawi sana huko Rumania na katika nchi nyingine za Ulaya Mashariki.
Nchini Marekani, harakati za kutafuta chanzo cha nuru nyangavu zaidi katika miaka ya 1800, zilifanya kikundi cha wanaume waanze kutafuta mafuta. Wanaume hao walikata kauli kwamba iliwabidi kuchimba mafuta ili wapate mafuta ya taa yanayotosheleza wateja. Kwa hiyo, katika mwaka wa 1859, kisima cha mafuta kilichimbwa huko Pennsylvania. Jitihada za kutafuta mafuta ya taa zikapamba moto.
-
-
Mafuta Hutoka Wapi?Amkeni!—2003 | Novemba 8
-
-
Mafuta Hutoka Wapi?
“NA KUWE na nuru.” Huko Marekani, katika karne ya 19, chanzo kingine cha nuru kilihitajiwa badala ya mafuta ya wanyama, ya nyangumi, na vitu vingine vilivyotokeza nuru hafifu. Suluhisho likawa nini? Mafuta! Yangepatikana wapi?
Mnamo mwaka wa 1859, kondakta wa gari la moshi aliyestaafu, Edwin L. Drake, alikuwa mtu wa kwanza kuchimba kisima cha mafuta chenye urefu wa meta 22 akitumia injini ya kale ya mvuke karibu na Titusville, Pennsylvania, Marekani. Mafuta yalianza kutumiwa sana wakati huo. Mafuta yalipogunduliwa katika sehemu nyingi za ulimwengu, kukawa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kisiasa. Mafuta yakawa chanzo bora cha nuru kilichokuwa kimetarajiwa kwa hamu ulimwenguni.
-