Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Sayansi Inapingana na Masimulizi ya Mwanzo?
    Amkeni!—2006 | Septemba
    • Kwa mfano, kabla ya “siku” ya kwanza, nuru ya jua, ambalo tayari lilikuwapo, ilizuiwa kwa njia fulani isiupige uso wa dunia. Labda ilikuwa ikizuiwa na mawingu mazito. (Ayubu 38:9) Kizuizi hicho kilianza kuondoka katika “siku” ya kwanza, na hivyo kuruhusu nuru ipenye kwenye anga la dunia.a

      Katika “siku” ya pili, anga lilizidi kuwa wazi, na hivyo kukawa na nafasi kati ya mawingu mazito yaliyokuwa juu na bahari iliyokuwa chini. Katika “siku” ya nne, anga lilikuwa wazi kabisa hatua kwa hatua hivi kwamba jua na mwezi zilionekana “katika anga la mbingu.” (Mwanzo 1:14-16) Kwa maneno mengine, mtu aliye duniani angeweza kuona jua na mwezi. Yote hayo yalitukia hatua kwa hatua.

  • Je, Sayansi Inapingana na Masimulizi ya Mwanzo?
    Amkeni!—2006 | Septemba
    • a Katika masimulizi ya matukio ya “siku” ya kwanza, neno la Kiebrania linalotafsiriwa nuru ni ʼohr, lakini kuhusu “siku” ya nne, neno linalotumiwa ni ma·ʼohrʹ, linalomaanisha vyanzo vya nuru.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki