Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha Kimbingu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na katika kiti cha ufalme zinatoka meme na sauti na ngurumo.” (Ufunuo 4:5a, NW) Lo! jinsi inavyokumbusha madhihirisho mengine yenye kutia hofu ya uwezo wa kimbingu wa Yehova! Mathalani, wakati Yehova ‘aliposhuka’ juu ya Mlima Sinai, Musa aliripoti hivi: “Katika siku ya tatu wakati ilipokuwa asubuhi, ikawa kwamba ngurumo na meme zikaanza kutukia, na wingu zito juu ya mlima na sauti kubwa sana ya pembe. . . . Wakati sauti ya pembe iliendelea kuwa kubwa zaidi na zaidi, Musa akaanza kunena, na Mungu wa kweli akaanza kujibu yeye kwa sauti.”—Kutoka 19:16-19, NW.

  • Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha Kimbingu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 13. Ni nini kinachoonyeshwa na picha ya meme zinazotoka katika kiti cha ufalme cha Yehova?

      13 Katika kipindi cha siku ya Bwana, Yehova hufanya nguvu na kuwapo kwake vidhihirike kwa njia yenye ukwezo mkubwa mno. La, si kwa umeme halisi, kwa kuwa Yohana anaona ishara. Basi, meme hizo zinawakilisha nini? Basi, mimeto ya umeme inaweza kunurisha, lakini inaweza pia kumpiga mtu mpaka kufa. Kwa hiyo, meme hizi zinazotoka kwenye kiti cha ufalme cha Yehova hufananisha kwa kufaa ile mimeto ya nuru ya elimu ambayo yeye amekuwa akiwapa watu wake kwa kuendelea na, hata la maana zaidi, jumbe zake za hukumu zenye moto.—Linga Zaburi 18:14; 144:5, 6; Mathayo 4:14-17; 24:27.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki