Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwe na Imani Kama ya Abrahamu!
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
    • Adui Ashambulia

      16. (a) Kwa nini maneno ya utangulizi ya Mwanzo 14:1 yanaonyesha kwamba jambo baya li karibu kutokea? (b) Kwa nini wafalme wanne wa mashariki walifanya uvamizi?

      16 “Ikawa siku za Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, na Kedorlaoma mfalme wa Elamuc na Tidali mfalme wa Goimu, walifanya vita.” Katika Kiebrania cha awali, maneno hayo ya utangulizi (“Ikawa siku za . . .”) yanaonyesha kwamba jambo baya li karibu kutokea na yanaashiria “kipindi cha majaribu kinacholeta baraka.” (Mwanzo 14:1, 2, NW, kielezi-chini) Jaribu hilo lilianza wakati wafalme hawa wanne wa mashariki pamoja na majeshi yao walipofanya uvamizi wao wenye uharibifu huko Kanaani. Walikuwa na lengo gani? Walitaka kukomesha uasi wa miji mitano ya Sodoma, Gomora, Adma, Seboimu, na Bela. Waliishinda miji hiyo, “wakakutana panapo bonde la Sidimu, kwenye Bahari ya Chumvi.” Loti na familia yake waliishi hapo karibu.—Mwanzo 14:3-7.

      17. Kwa nini kutekwa kwa Loti kulijaribu imani ya Abramu?

      17 Wafalme wa Kanaani walizuia wavamizi hao kwa ujasiri, lakini wakashindwa vibaya sana. “Basi, wale walioshinda, wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora, kadhalika na mazao yao, wakaenda zao. Walimteka hata Loti, mwana wa nduguye Abramu aliyekuwa anakaa Sodoma, pamoja na mali yake, wakaenda zao.” Muda si muda, habari za matukio hayo yenye kuhuzunisha zikamfikia Abramu: “Mtu mmoja aliyeponyoka, akaenda kumwarifu yule Mwebrania Abramu ambaye alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mwamori Mamre. Mamre alikuwa ndugu yake Eshkoli na Aneri. Wote walikuwa wamefanya agano na Abramu. [Hivyo Abramu akapata] habari kwamba mpwa wake amechukuliwa mateka.” (Mwanzo 14:8-14, BHN) Ni jaribu la imani lililoje! Je, Abramu angekuwa na chuki kuelekea mpwa wake kwa kuwa alichukua sehemu ya nchi iliyokuwa bora zaidi? Kumbuka pia kwamba wavamizi hawa walitoka Shina, nchi yake ya asili. Kupigana nao kungefanya isiwezekane kwake kurudi nyumbani. Isitoshe, je, Abramu angeweza kufanya chochote dhidi ya jeshi ambalo majeshi yote ya Kanaani hayakuweza kuyashinda?

      18, 19. (a) Abramu aliwezaje kumwokoa Loti? (b) Ni nani aliyepata sifa kwa ushindi huo?

      18 Kwa mara nyingine, Abramu alimtumaini Yehova kabisa. ‘Akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani. Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Demeski. Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Loti nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.’ (Mwanzo 14:14-16) Kwa kuonyesha imani yenye nguvu katika Yehova, Abramu alipata ushindi kwa jeshi lake lililokuwa dogo sana, akamwokoa Loti na familia yake. Wakati huo ndipo Abramu alipokutana na Melkizedeki, mfalme-kuhani wa Salemu. “Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.”—Mwanzo 14:18-20.

      19 Naam, Yehova ndiye aliyekuwa mshindi. Kwa mara nyingine tena, Abramu aliokolewa na Yehova kwa sababu ya imani yake.

  • Msife Moyo Katika Kufanya Lililo Bora
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
    • Shambulio la Moja kwa Moja

      4. Shetani ametumiaje mashambulio ya moja kwa moja ili kujaribu kuvunja uaminifu-maadili wa watu wa Mungu?

      4 Bila shaka maisha ya Abrahamu yanaonyesha “majaribu ya namna mbalimbali” ambayo Mkristo anaweza kukabili leo. Kwa mfano, ilimbidi kuchukua hatua dhidi ya wavamizi wa Shina. (Mwanzo 14:11-16) Si ajabu kwamba Shetani anaendelea kutushambulia moja kwa moja kupitia mnyanyaso. Tangu Vita ya Pili ya Ulimwengu imalizike, serikali za nchi nyingi zimepiga marufuku kazi ya Kikristo ya Mashahidi wa Yehova ya kuelimisha watu. Kitabu 2001 Yearbook of Jehovah’s Witnesses charipoti juu ya ujeuri ambao Wakristo huko Angola walitendewa na adui. Kwa kumtegemea Yehova, ndugu zetu katika nchi hizo wamekataa katakata kuacha kazi ya Kikristo! Badala ya kuchukua hatua ya ujeuri au ya uasi, ndugu hao wameendelea kwa busara na kazi yao ya kuhubiri.—Mathayo 24:14.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki