-
Upendo wa Kikristo Wakati wa VolkenoAmkeni!—2000 | Aprili 22
-
-
Makutaniko ya Mashahidi wa Yehova yalipeleka chakula. Shahidi mmoja alitoa matofali 1,000 ya saruji. Mwingine alipanga ununuzi wa mabati ya kuezeka kwa bei nafuu. Na mwingine alitembea kilometa 16 kupata mbao. Mwanamume mmoja kijana ambaye alikuwa ameweka pesa akibani ili kulipia mahari kwa wale ambao wangekuwa wakwe zake, aliahirisha harusi na kutumia pesa hizo kurekebisha msumeno wake wa mnyororo. Kisha akaenda msituni, ambapo kwa majuma matatu alikata magogo ya nyumba nzima! Ndugu vijana Wakristo walibeba mbao kwenye vichwa vyao kwa umbali wa kilometa tano, ambapo gari la kubebea mizigo lilizichukua.
Ujenzi ukaanza Aprili 24 wakati wajitoleaji 60 walipokutana penye msiba. Wakati wa miisho-juma iliyofuata, idadi iliongezeka hadi kufikia kilele cha watu 200. Mashahidi wawili wenye kazi za wakati wote walikuja baada ya kazi yao ya kawaida siku hiyo nao wakajenga hadi baada ya saa sita usiku. Shahidi mmoja kutoka Douala alikwenda kazini alikoajiriwa asubuhi yote; kisha akasafiri kwa pikipiki yake kilometa 70 naye akafanya kazi mpaka saa sita usiku kabla ya kurudi nyumbani. Nyumba sita zilikamilishwa kwa muda usiozidi miezi miwili. Wakati uleule, kutaniko la Buea liliendelea kufanya mikutano katika makao ya faragha, ingawa hudhurio la mkutano lilikuwa maradufu ya idadi ya washiriki wa kutaniko.
-
-
Upendo wa Kikristo Wakati wa VolkenoAmkeni!—2000 | Aprili 22
-
-
Baada ya kuona mojawapo ya nyumba zilizojengwa na akina ndugu, mwanamume mmoja kutoka katika Baraza la Mkoa la Kilimo alisema: “Nyumba hiyo yenyewe ni ushahidi mkubwa . . . , wonyesho wa upendo.” Mwalimu mmoja alieleza hivi: “Sijapata kuona kamwe jambo kama hilo maishani mwangu. . . . Hiyo kwa kweli ni ishara ya Ukristo wa kweli.”
Wale walionufaika binafsi vilevile walieleza vivyo hivyo. Timothy, mwenye umri wa miaka 65 na mgonjwa-mgonjwa, aliandika: “Kila mara tuangaliapo nyumba yetu mpya, machozi ya shangwe hututiririka. Twaendelea kumshukuru Yehova kwa yale ambayo ametufanyia.” Mjane mwenye watoto wanne ambaye si mmoja wa Mashahidi wa Yehova alipoteza kila kitu nyumba yao ilipoporomoka. Kisha wale walioajiriwa kumsaidia wakaiba vifaa vyake vya kuezekea paa. Wajitoleaji Mashahidi walimsaidia. Yeye alisema hivi: “Sijui nishukuruje. Moyo wangu umejaa shangwe.” Elizabeth, mke wa mzee Mkristo, alisema hivi: “Ninafurahi kwamba kuna upendo katika tengenezo la Yehova. Yaonyesha kwamba twamtumikia Mungu aliye hai.”
-