-
Yehova Hubariki Ibada SafiUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
20. Yerusalemu limebarikiwaje kwa “kijito kifurikacho,” nyakati za kale na za kisasa pia?
20 Unabii unaendelea kusema hivi: “BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa [“ubavuni,” “NW”]; na juu ya magoti mtabembelezwa.” (Isaya 66:12)
-
-
Yehova Hubariki Ibada SafiUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
21. Ni faraja ya aina gani inayotabiriwa kwa maneno ya ufananisho yenye kuvutia?
21 Andiko la Isaya 66:12 pia linataja semi zitumiwazo na mama-mzazi kuonyesha upendo. Semi hizo zinahusu kubembeleza mtoto kwa kumpakata magotini na kumbeba kwa kumweka ubavuni. Katika mstari unaofuata, wazo la namna hiyo linaelezwa kwa maoni tofauti yanayostahili kufikiriwa. “Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu.” (Isaya 66:13) Sasa mtoto huyo ni “mtu,” mtu mzima. Lakini mama yake hajaacha kutamani kumfariji wakati wa msononeko.
22. Yehova anaonyeshaje wororo na uthabiti wa upendo wake?
22 Kwa njia hiyo ya kuvutia, Yehova anaonyesha jinsi anavyowapenda watu wake kwa uthabiti na wororo mwingi. Hata upendo imara kabisa wa mama-mzazi unakuwa kitu kidogo sana unapolinganishwa na upendo wa kina kirefu ambao Yehova huwaonyesha watu wake waaminifu. (Isaya 49:15) Ni muhimu kama nini Wakristo wote waonyeshe sifa hiyo ya Baba yao wa kimbingu! Mtume Paulo aliionyesha, na hivyo akawaachia wazee wa kutaniko la Kikristo mfano mzuri. (1 Wathesalonike 2:7) Yesu alisema kwamba upendo wa kidugu ndio ungekuwa alama kuu ya kutambulisha wafuasi wake.—Yohana 13:34, 35.
-