Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wahasmonia na Hali Waliyoacha
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Juni 15
    • John Hyrcanus, mwana aliyesalia wa Simon alionywa juu ya jaribio la kumwua. Aliwakamata watu ambao wangemwua na kuchukua uongozi na ukuhani mkuu, vyeo vilivyokuwa vya babake.

      Upanuzi Zaidi na Ukandamizaji

      Mwanzoni, John Hyrcanus alikabili vitisho vikali kutoka kwa majeshi ya Siria, lakini katika mwaka wa 129 K.W.K., ufalme wa nasaba ya Seleuko ukashindwa kwenye vita muhimu walivyopigana na Waparthia. Kuhusiana na matokeo ya vita hivyo vya Waparthia na ufalme wa nasaba ya Seleuko, msomi mmoja Myahudi Menahem Stern aliandika: “Mpangilio wote wa ufalme uliporomoka.” Hivyo Hyrcanus “akaweza kuliweka huru kisiasa eneo lote la Yudea na kuanza kulipanua kuelekea pande mbalimbali.” Na alilipanua kwelikweli.

      Sasa kukiwa hakuna tisho lolote lenye kumzuia kutoka Siria, Hyrcanus alianza kuvamia maeneo yaliyokuwa nje ya Yudea, na kuyatawala. Walilazimisha wakazi wa maeneo hayo kugeuza imani yao na kufuata Dini ya Wayahudi la sivyo majiji yao yangeharibiwa kabisa. Walifanya hivyo na Waedomu. Kuhusu jambo hilo Stern alisema: “Kugeuzwa imani kwa Waedomu kulikuwa kwa pekee, kwa kuwa si watu wachache tu waliogeuzwa imani bali jamii nzima.” Mojawapo ya maeneo yaliyovamiwa ni Samaria, ambako Hyrcanus aliharibu kabisa hekalu la Samaria kwenye Mlima Gerizimu. Akionyesha jambo lililo kinyume cha sera hiyo ya wafalme wa nasaba ya Wahasmonia ya kuwalazimisha watu kubadili imani yao, mwanahistoria Solomon Grayzel aliandika hivi: “Mjukuu wa Mattathias [baba ya Judah Maccabee] alikuwa anavunja kanuni, yaani, uhuru wa ibada ambao kizazi kilichopita kilikuwa kimeuhifadhi vizuri.”

      Mafarisayo na Masadukayo Watokea

      Anapoandika juu ya utawala wa Hyrcanus, ndipo Josephus kwanza anaandika juu ya uvutano unaozidi wa Mafarisayo na Masadukayo.

  • Wahasmonia na Hali Waliyoacha
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Juni 15
    • Josephus asimulia kwamba mwanzoni John Hyrcanus alikuwa mwanafunzi wa Mafarisayo na aliwaunga mkono. Hata hivyo, baadaye Mafarisayo walimkemea kwa kutoacha ukuhani wa cheo cha juu, jambo lililofanya afarakane nao kabisa. Hyrcanus alipiga marufuku sheria za kidini za Mafarisayo. Ili kuwaadhibu zaidi Mafarisayo, aliwaunga mkono Masadukayo waliokuwa wapinzani wao wa kidini.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki