-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
na yeye ataenda nje kuongoza vibaya yale mataifa katika kona nne za dunia, Gogu na Magogu, kukusanya hayo pamoja kwenye vita. Hesabu ya hawa ni kama mchanga wa bahari.
-
-
Kuponda Kichwa cha NyokaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
22. (a) Ni nini kinachoonyeshwa na usemi “yale mataifa katika kona nne za dunia”? (b) Kwa nini waasi huitwa “Gogu na Magogu”?
22 Biblia huwaita waasi hawa “mataifa katika kona nne za dunia.” Hii haimaanishi kwamba aina ya binadamu itakuwa imekwisha gawanyikana-gawanyikana tena na kuwa mataifa yaliyo pekee. Inaonyesha tu kwamba hawa watajitenga wenyewe kutoka kwa wale washikamanifu, na waadilifu wa Yehova na kudhihirisha roho ile ile mbaya ambayo mataifa yanaonyesha leo. Wao ‘watafikiria njama yenye kudhuru,’ kama alivyofanya Gogu wa Magogu katika unabii wa Ezekieli, wakiwa na mradi wa kuharibu serikali ya kitheokrasi iliyo duniani. (Ezekieli 38:3, 10-12, NW) Kwa sababu hiyo, wao huitwa “Gogu na Magogu.”
-