Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maendeleo Makubwa Nchini Malawi—Majumba 1,000 ya Ufalme!
    Amkeni!—2012 | Mei
    • ✔ “Ujenzi wa jengo jipya la ibada, pamoja na upendo na umoja wa Mashahidi wa Yehova, ni kama kito katika jamii, mfano mzuri wa kuigwa na makanisa mengine.”—Chifu wa kijiji cha Chabwenzi.

      ✔ “Jambo linalonivutia zaidi kuhusu Mashahidi wa Yehova ni umoja wao. Tulianza kujenga kanisa letu miaka kumi iliyopita, lakini bado ujenzi unaendelea—na haionekani kama utakwisha hivi karibuni. Ningependa kuwashukuru kwa kujenga jumba maridadi kama hili katika eneo letu.”—Mzee wa kijiji cha Chigwenembe.

      ✔ “Inasisimua kuona jinsi mnavyofanya kazi. Mnajenga haraka na kwa utaratibu mzuri! Lazima muwe mna umoja kwelikweli.”—Chifu wa kijiji cha Chiuzira.

  • Maendeleo Makubwa Nchini Malawi—Majumba 1,000 ya Ufalme!
    Amkeni!—2012 | Mei
    • Hata hivyo, Bi. Liness Chikaoneka ambaye ni mzee wa kijiji, alijitahidi sana kuwashawishi maofisa ili watie sahihi stakabadhi hizo.”

      Siku moja, Bi. Chikaoneka aliandamana na mzee mmoja wa kutaniko alipokuwa akipeleka stakabadhi ili zitiwe sahihi. “Ninataka Mashahidi wajenge Jumba la Ufalme katika kijiji changu,” akamwambia ofisa. “Wao ni watu wazuri. Sijawahi kushughulikia shtaka lolote kuwahusu katika mahakama yangu ya kijiji.” Ofisa huyo alitia sahihi stakabadhi hizo.

      Bi. Chikaoneka alifurahi sana wakati Jumba hilo la Ufalme lilipowekwa wakfu. Alisema hivi: “Nina furaha na ninajivunia kuwa na jengo hili maridadi katika kijiji changu!”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki