Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Baadhi ya wakuu wa serikali wasiopendelea upande wowote hawakukubali bila kuuliza maswali yale mashtaka ya kikatili yaliyofanywa na makasisi wa Jumuiya ya Wakristo dhidi ya Mashahidi. Ndivyo ilivyokuwa kwa habari ya kamishna wa polisi katika Nyasaland (sasa ni Malawi) aliyejifanya asiweze kutambulika akaenda kwenye mikutano ya Mashahidi wenyeji ili apate kujionea mwenyewe walikuwa watu wa aina gani. Alivutiwa vizuri. Wakati kibali kilipotolewa na serikali ili kuwa na mwakilishi Mzungu mkazi, Bert McLuckie na baadaye ndugu yake Bill walitumwa huko katika miaka ya katikati ya 1930. Waliendelea kuwasiliana na polisi na makamishna wa wilaya ili maofisa hao waweze kuwa na uelewevu ulio wazi wa utendaji wao na ili wasichanganyikiwe kati ya Mashahidi wa Yehova na yoyote ya zile harakati ziitwazo Watchtower kibandia. Wakati huohuo, walifanya kazi kwa saburi, pamoja na Gresham Kwazizirah, Shahidi mwenyeji aliyekomaa, ili wasaidie mamia ya wale waliotaka kushirikiana na makutaniko watambue kwamba ukosefu wa adili kingono, matumizi mabaya ya vileo, na ushirikina ni mambo yasiyofaa maishani mwa Mashahidi wa Yehova.—1 Kor. 5:9-13; 2 Kor. 7:1; Ufu. 22:15.

  • Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Hatua kwa hatua hesabu ya Mashahidi wa Yehova ilikua katika sehemu hii ya shamba la ulimwengu. Wengine walijiunga na wale wachache walioanzisha kazi barani Afrika mapema katika karne hii ya 20, na kufikia 1935 walikuwa 1,407 katika bara la Afrika walioripoti kuwa walishiriki katika kazi ya kutoa ushahidi juu ya Ufalme wa Mungu. Hesabu kubwa zao zilikuwa katika Afrika Kusini na Nigeria. Vikundi vingine vikubwa vilivyojitambulisha kuwa Mashahidi wa Yehova vilikuwa katika Nyasaland (sasa ni Malawi), Rhodesia Kaskazini (sasa ni Zambia), na Rhodesia Kusini (sasa ni Zimbabwe).

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki