Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Malasia

      Wakati wa utawala wa kikoloni wa Uingereza, maelfu ya vibarua waliletwa Malasia kufanya kazi kwenye mashamba ya miti ya mpira. Walijengewa vijiji katika mashamba hayo, na vijiji vingi bado vipo. Vingi kati ya vijiji hivyo havifikiki kwa urahisi na hata havionyeshwi kwenye ramani. Ndugu katika kutaniko moja walipata kijiji fulani katika shamba la miti ya mpira walipokuwa wakihubiri katika eneo ambalo halijagawiwa yeyote. Vijana wawili wenye umri wa karibu miaka 20, ambao tayari walikuwa wamechukua magazeti, walipendezwa sana na kazi ya kuhubiri ya ndugu hao. Vijana hao walijitolea kuwaonyesha vijiji vingine. Tofauti na ndugu hao, wao walijua eneo hilo vizuri sana. Walipanda pikipiki zao na kuongoza gari za ndugu hao. Walipita kwenye mashamba wakifuata vijia na barabara zenye matope, na nyakati nyingine iliwachukua muda wa dakika 45 hivi kutoka kijiji kimoja hadi kingine. Waliwaongoza ndugu hao kwenye mashamba ambayo hayakuwa yamewahi kutembelewa na Mashahidi. Ndugu hao walipokuwa wakihubiri, vijana hao waliwahimiza wanavijiji wachukue magazeti na kuhakikisha kwamba wameyasoma. Kwa ujumla, waliwapeleka ndugu hao kwenye vijiji vitatu vilivyokuwa mbali. Msaada wa vijana hao wasio na ubinafsi uliwawezesha ndugu kuwahubiria watu ambao hawakuwa wamewahi kusikia habari njema. Katika siku mbili walizokuwa huko, yaani, Jumamosi na Jumapili (Siku ya Yenga), wahubiri 50 kutoka kutaniko hilo waliachia watu magazeti zaidi ya 5,000.

  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 54]

      Kumhubiria mwanamke Mhindi katika shamba la mipira

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki