Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhifadhi Joto Katika Theluji
    Amkeni!—2008 | Februari
    • Maisha Chini ya Theluji

      Wakipitia mitaro mingi iliyo chini ya theluji, wanyama fulani wadogo wenye manyoya wanaendelea na shughuli zao, wakati mwingi wakitafuta chakula. Wanyama hao wanatia ndani lemming, panyabuku, na aina ya fuko ambao hula wadudu nyakati za usiku. Nao panya wengine wanaonekana wakikimbia juu ya theluji wakitafuta beri, njugu, mbegu, na maganda ya miti michanga.

      Wanyama wadogo wanawezaje kudumisha joto la mwili linalofaa? Zaidi ya kuwa na manyoya mengi, wanyama wengi pia hutokeza joto jingi kwa kuyeyusha chakula haraka. Kwa hiyo, ili waweze kutokeza joto jingi wanahitaji kula chakula kingi. Kwa mfano, kila siku panya hula kiasi cha wadudu kinachokaribia uzito wao. Nao aina fulani ya panya wadogo wanakula chakula kingi hata zaidi! Kwa hiyo, wanatumia karibu wakati wao wote kutafuta chakula.

      Panya hao wanawindwa sana na wanyama fulani kutia ndani bundi na jamii kadhaa za kicheche, na ermine. Vicheche ni wanyama wembamba na wepesi, kwa hiyo ni rahisi kwao kupitia chini ya theluji katika vijia vilivyofichika wanapotafuta chakula. Wao huwinda hata sungura, wanyama wanaowazidi kwa ukubwa.

  • Kuhifadhi Joto Katika Theluji
    Amkeni!—2008 | Februari
    • Ili wasife njaa katika majira ya baridi kali, wanyama wengi hutumia mafuta waliyokusanya katika miezi yenye joto. Lakini kwa kawaida wao hupata kiasi fulani cha chakula. Kwa mfano, kongoni hula matawi ya miti michanga hasa misonobari. Kindi hula mbegu walizokusanya na kuhifadhi, nao sungura-mwitu hula maganda ya miti michanga, matawi, na majani.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki