Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uhai
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Je, wanadamu waliumbwa waishi miaka michache tu kisha wafe?

      Mwa. 2:15-17: “Yehova Mungu akamchukua mtu [Adamu] na kumweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Pia Yehova Mungu akamwekea mtu amri hii: ‘Matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula mpaka ushibe. Lakini kuhusu matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula, utakufa hakika.’” (Mungu alipokuwa akisema juu ya kifo, hakusema kwamba hakingeweza kuepukika, bali kwamba kingetokana na dhambi. Alikuwa akimhimiza Adamu akiepuke. Linganisha na Waroma 6:23.)

      Mwa. 2:8, 9: “Yehova Mungu akapanda bustani katika Edeni, kuelekea mashariki, na hapo akamweka mtu ambaye alikuwa amemfanya. Hivyo Yehova Mungu akachipusha katika nchi kila mti wenye kutamanika kwa macho ya mtu na ulio mwema kwa ajili ya chakula na pia mti wa uzima katikati ya bustani.” (Baada ya dhambi ya Adamu, watu wawili wa kwanza walifukuzwa kutoka Edeni ili wasipate kula kutokana na mti wa uzima, kulingana na Mwanzo 3:22, 23. Kwa hiyo, inaonekana kwamba ikiwa Adamu angeendelea kumtii Muumba wake, mwishowe Mungu angemruhusu ale kutokana na mti huo ili kuonyesha kwamba anastahili kuishi milele. Kuwapo kwa mti huo wa uzima katika Edeni kulionyesha tazamio hilo.)

      Zab. 37:29: “Waadilifu wenyewe wataimiliki dunia, nao watakaa milele juu yake.” (Ahadi hiyo inaonyesha wazi kwamba kusudi la msingi la Mungu kuhusu dunia na wanadamu halijabadilika.)

  • Uhai
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Je, kuna chochote katika mwili wa mwanadamu kinachothibitisha kwamba alikusudiwa aishi milele?

      Wengi wametambua kwamba ubongo wa mwanadamu una uwezo mkubwa kuliko jinsi unavyotumiwa katika maisha yetu ya sasa, tuwe tunaishi hadi umri wa miaka 70 au hata 100. Encyclopædia Britannica inasema kwamba ubongo wa mwanadamu “una uwezo mkubwa kuliko ule unaoweza kutumiwa katika muda wa maisha ya mtu mmoja.” (1976, Buku la 12, uku. 998) Mwanasayansi Carl Sagan hutaarifu kwamba ubongo wa mwanadamu unaweza kuhifadhi habari “inayoweza kujaa mabuku kama milioni ishirini, jumla ya yale yaliyo katika maktaba kubwa zaidi za ulimwengu.” (Cosmos, 1980, uku. 278) Kuhusu uwezo wa ubongo wa mwanadamu wa “kuhifadhi mambo,” mwanakemia Isaac Asimov aliandika kwamba “una uwezo kamili wa kujifunza chochote na kukumbuka chochote ambacho mwanadamu anaweza kujifunza—na mara bilioni zaidi ya kiasi hicho, pia.”—The New York Times Magazine, Oktoba 9, 1966, uku. 146. (Kwa nini ubongo wa mwanadamu una uwezo huo ikiwa haukupaswa kutumiwa? Je, si jambo linalopatana na akili kwamba wanadamu, kwa kuwa wana uwezo wa kujifunza milele, waliumbwa waishi milele?)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki