Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Januari 15
    • Muda mfupi baada ya kukombolewa kutoka Misri, Waisraeli walianza kulalamika kuhusu chakula. Basi, Yehova akawaandalia mana. (Kutoka 12:17, 18; 16:1-5) Wakati huo, Musa alimwagiza Haruni hivi: “Chukua mtungi, uweke omeri moja kamili ya mana na kuiweka mbele za Yehova iwe kitu cha kuwekwa katika vizazi vyenu vyote.” Kisha simulizi hilo linasema: “Sawasawa na vile Yehova alivyokuwa amemwamuru Musa, Haruni akaiweka mbele ya ule Ushuhuda [hifadhi ya hati muhimu] iwe kitu cha kuwekwa.” (Kutoka 16:33, 34) Ingawa ni wazi kwamba Haruni aliweka mana katika mtungi wakati huo, ilibidi angoje Musa alitengeneze Sanduku na aingize yale mabamba kabla ya kuweka mtungi huo mbele ya ule Ushuhuda.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Januari 15
    • Mungu aliandaa mana wakati Waisraeli walipokaa nyikani miaka 40. Mana haikuandaliwa tena ‘walipoanza kula mazao ya nchi’ ya ahadi. (Yoshua 5:11, 12) Fimbo ya Haruni iliwekwa ndani ya sanduku la agano kwa kusudi fulani, yaani, ili iwe ishara au uthibitisho wa kukishutumu kizazi kilichoasi. Hilo linaonyesha kwamba fimbo hiyo ilibaki humo angalau kwa muda ambao Waisraeli walisafiri nyikani. Kwa hiyo, ni jambo la akili kukata kauli kwamba muda fulani baada ya Waisraeli kuingia Nchi ya Ahadi na kabla ya kuwekwa wakfu kwa hekalu la Sulemani, fimbo ya Haruni na mtungi wa dhahabu wa mana viliondolewa kwenye sanduku la agano.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki