-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
11. Kwa nini ilifaa sana yule Mchungaji Mkuu ayaonye makundi juu ya miendo iliyokuwa ikisitawi?
11 Hata hivyo, mtume Paulo alikuwa ametabiri kwamba kungekuwako uasi-imani miongoni mwa Wakristo wapakwa-mafuta, na jumbe za Yesu huonyesha kwamba katika umri wa uzee wa Yohana uasi-imani huu ulikuwa tayari ukisitawi. Yohana alikuwa wa mwisho wa wale waliokuwa wakitenda wakiwa kizuizi katika jaribio hili la kupindukia la Shetani la kufisidi ile mbegu ya mwanamke. (2 Wathesalonike 2:3-12; 2 Petro 2:1-3; 2 Yohana 7-11) Kwa hiyo ulikuwa wakati unaofaa kwa Mchungaji Mkuu wa Yehova kuandikia wazee katika makundi, akiwaonya juu ya miendo iliyokuwa ikisitawi na kuwatia moyo wale wenye mioyo iliyo sawa wasimame imara kwa ajili ya uadilifu.
-
-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Kweli kweli, viongozi wa dini za Jumuiya ya Wakristo wamekuwa ndio washiriki wenye kutokeza zaidi wa ile mbegu ya Shetani. Akisema juu ya hao kuwa ‘yule mtu wa uasi-sheria,’ mtume Paulo alitabiri kwamba ‘kuwapo kwao ni kulingana na utendaji wa Shetani pamoja na kila kazi yenye nguvu na ishara za kusema uwongo na maajabu na pamoja na kila danganyo lisilo la uadilifu.’—2 Wathesalonike 2:9, 10, NW.
16. (a) Viongozi wa Jumuiya ya Wakristo walionyesha uchukivu wa pekee kwa nani? (b) Ni jambo gani lililotukia katika Jumuiya ya Wakristo katika kile kipindi cha zile Enzi za Katikati? (c) Je! ule uasi au Mapinduzi Makuu ya Kiprotestanti, yalibadili njia za uasi-imani za Jumuiya ya Wakristo?
16 Huku wakidai kuwa wachungaji wa kundi la Mungu, viongozi wa Jumuiya ya Wakristo, wa kidini na wa kiserikali, walionyesha uchukivu wa pekee kwa yeyote aliyejaribu kutia moyo usomaji wa Biblia au yeyote aliyefichua mazoea yao yasiyo ya kimaandiko. John Hus na mtafsiri Biblia William Tyndale, walinyanyaswa na wakauawa kwa sababu ya imani yao. Katika kile kipindi chenye kutiwa giza cha Enzi za Katikati, utawala wa wenye kuasi imani ulifikia upeo wao kwa lile Baraza la Kuhukumia Wazushi wa Kidini lenye ukatili mwingi la Kikatoliki. Watu wowote waliopinga mafundisho au mamlaka ya kanisa walikandamizwa bila rehema, na maelfu yasiyohesabika ya wale walioitwa eti wazushi wa kidini waliteswa-teswa mpaka kifo au wakachomwa penye nguzo. Hivyo Shetani alijitahidi kuhakikisha kwamba mbegu yoyote ya kweli ya tengenezo la Yehova lililo mfano wa mwanamke ingepondwa-pondwa kwa haraka sana. Wakati ule uasi au Mapinduzi Makuu ya Kiprotestanti yalipotukia (kuanzia 1517 na kuendelea), makanisa mengi ya Kiprotestanti yalidhihirisha roho ile ile ya kutovumilia. Hayo vilevile yakawa yenye hatia ya damu kwa kuwaua kwa sababu ya imani yao wale wote waliojaribu kuwa washikamanifu kwa Mungu na Kristo. Kweli kweli, “damu ya watakatifu” ilimwagwa kwa wingi sana!—Ufunuo 16:6; linga Mathayo 23:33-36.
-