-
Historia Inayopendeza ya SiriaAmkeni!—2003 | Februari 8
-
-
Jiji la kale la Mari lilikuwa umbali wa kilometa 25 kuelekea kusini-mashariki kutoka Dura-Europos. Jiji hilo lililokuwa tajiri kibiashara liliharibiwa na Mfalme Hammurabi wa Babiloni katika karne ya 18 K.W.K. Mabamba zaidi ya 15,000 ya udongo yenye maandishi yamepatikana katika jumba la mfalme la jiji hilo. Hayo yanaeleza mengi kuhusu maisha ya wakati huo.
Majeshi ya Hammurabi walipoharibu jiji hilo, walibomoa kuta za juu na kujaza vyumba vya chini kwa matofali na udongo. Kwa hiyo, michoro ya kuta, sanamu, vyombo vya udongo, na vitu vingine vingi vilihifadhiwa hadi wanaakiolojia Wafaransa walipogundua jiji hilo mwaka wa 1933. Vitu hivyo vimo katika majumba ya makumbusho huko Damasko na Aleppo, na vilevile huko Louvre, Paris.
-
-
Historia Inayopendeza ya SiriaAmkeni!—2003 | Februari 8
-
-
[Picha katika ukurasa wa 26]
Mari
-