Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Faraja kwa Watu wa Mungu
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 13, 14. Maneno “Rahabu” na ‘yule joka wa baharini’ yanafananisha nini, naye ‘atakatwa-katwa’ na ‘kuchomwa’ kwa njia gani?

      13 Isaya anasema hivi kana kwamba anamwita Yehova achukue hatua kuwatetea watu Wake walio mateka: “Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; amka kama katika siku zile za kale, katika vizazi vile vya zamani. Si wewe uliyemkata-kata Rahabu? Uliyemchoma yule joka [“wa baharini,” “NW”]?

  • Faraja kwa Watu wa Mungu
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Maneno “Rahabu” na ‘yule joka wa baharini’ yanarejezea Misri ikiwa chini ya Farao wake aliyepinga lile tukio la Kutoka kwa Israeli nchini Misri. (Zaburi 74:13; 87:4; Isaya 30:7) Misri ilifanana na joka kubwa ajabu, kichwa chake kikiwa kwenye Delta ya Mto Naili, na kiwiliwili chake kirefu kikiinuka juu mamia ya kilometa katika bonde la Mto Naili lenye rutuba. (Ezekieli 29:3) Lakini joka hilo kubwa lilikatwa vipande vipande Yehova alipomimina Mapigo Kumi juu yake. Lilidungwa, likajeruhiwa vibaya, likadhoofishwa jeshi lake lilipoangamizwa katika maji mengi ya Bahari Nyekundu. Naam, Yehova alizionyesha nguvu za mkono wake katika shughuli zake na Misri. Sembuse yeye kuwa tayari kuwapigania watu wake waliopelekwa uhamishoni Babiloni!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki