-
Marko ‘Mwenye Faida kwa Ajili ya Huduma’Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 15
-
-
Mtume Petro aliandika barua yake ya kwanza kati ya mwaka wa 62 na 64 W.K. Aliandika hivi: “Mwanamke aliye katika Babiloni . . . anawatumia ninyi salamu zake, na vilevile Marko mwanangu.” (1 Pet. 5:13) Kwa hiyo, Marko alisafiri mpaka Babiloni ili kutumika pamoja na mtume Petro ambaye miaka iliyotangulia alihudhuria mikutano ya Kikristo katika nyumba ya mama ya Marko.
-
-
Marko ‘Mwenye Faida kwa Ajili ya Huduma’Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 15
-
-
Ingawa kitabu cha pili cha Injili hakimtaji mwandikaji, mapokeo ya zamani yanadai kwamba Marko ndiye aliyeandika kitabu hicho na alipata habari kutoka kwa Petro. Kwa kweli, Petro alishuhudia karibu kila jambo ambalo Marko aliandika.
-