-
Tumeungana Katika Utumishi wa Mungu Kupitia Nyakati Nzuri na MbayaMnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
Miezi minne baada ya kufika Tahiti, tulipanda mashua ndogo iliyojazwa mizigo ya nazi zilizokauka. Siku tano baadaye tulifika kwenye mgawo wetu mpya—kisiwa cha Nuku Hiva katika Visiwa vya Marquesas. Watu wapatao 1,500 waliishi katika kisiwa hicho, lakini hakukuwa na ndugu. Sisi tu.
Hali zilikuwa za kikale wakati huo. Tuliishi katika nyumba ndogo iliyotengenezwa kwa saruji na mianzi. Hakukuwa na umeme. Tulikuwa na mfereji wa maji uliokuwa ukifanya kazi nyakati nyingine, lakini maji yalikuwa yenye tope-tope. Mara nyingi, tulitumia maji ya mvua tuliyodunduliza kwenye tangi. Hakukuwa na barabara zilizotengenezwa vizuri, kulikuwa na njia za mchanga tu.
Ili kufika sehemu za mbali za kisiwa, ilitubidi tukodishe farasi. Matandiko yalifanyizwa kwa mbao—yasiyostarehesha kabisa, hasa kwa Babette, ambaye hakuwa amepata kuendesha farasi kamwe. Tulikuwa tukibeba mundu ili kukata mianzi iliyokuwa ikianguka njiani. Lilikuwa badiliko kubwa na maisha ya Ufaransa.
Tulifanya mikutano ya Jumapili, ijapokuwa ni sisi wawili tu tuliohudhuria. Mara ya kwanza, hatukuwa na mikutano mingine kwa kuwa tulikuwa sisi wawili tu. Badala yake tulisoma habari ya mkutano pamoja.
Baada ya miezi michache, tuliamua kwamba haikuwa vizuri twendelee kwa njia hii. Michel asimulia: “Nilimwambia Babette, ‘Lazima tuvae vizuri. Wewe keti pale, nami nitaketi hapa. Nitaanza kwa sala, kisha tutakuwa na mkutano wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi na Mkutano wa Utumishi. Nitauliza maswali, nawe utajibu, hata kama wewe tu ndiye mtu aliye chumbani.’ Ilikuwa vizuri kufanya hivyo kwa sababu ni rahisi kuwa walegevu kiroho wakati ambapo hakuna kutaniko.”
Ilichukua muda kupata watu ili waje kwenye mikutano yetu ya Kikristo. Sisi wawili tulikuwa peke yetu kwa miezi minane ya kwanza. Baadaye, mtu mmoja, wawili, au wakati mwingine watatu walijiunga nasi. Mwaka mmoja, sisi wawili tu tulianzisha ule mwadhimisho wa kila mwaka wa Mlo wa Jioni wa Bwana. Baada ya dakika kumi, watu wengine wakaja, kwa hiyo nikatua na kuanza hotuba tena.
-
-
Tumeungana Katika Utumishi wa Mungu Kupitia Nyakati Nzuri na MbayaMnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
-
-
Tulijifunza subira katika Nuku Hiva. Ilitubidi tungojee kila kitu ila mahitaji yetu ya lazima zaidi. Kwa mfano, kama ulitaka kitabu, uliandika, kisha ungoje kwa miezi miwili au mitatu kabla hakijafika.
-