-
Kumjua Mungu Huimarisha FamiliaMnara wa Mlinzi—2005 | Mei 15
-
-
“UKUTA wa Berlin.” Hivyo ndivyo wenzi fulani wa ndoa huko Argentina walivyouita ukuta halisi ambao walijenga ili kugawanya nyumba yao mara mbili! Walikuwa wamekosana kabisa na walichukiana sana.
-
-
Kumjua Mungu Huimarisha FamiliaMnara wa Mlinzi—2005 | Mei 15
-
-
Kwa mfano, fikiria wale wenzi wa ndoa huko Argentina ambao wametajwa mwanzoni mwa makala hii. Baada ya kujifunza Biblia na Mashahidi wa Yehova kwa miezi mitatu, wote wawili walianza kutii mashauri ya Biblia yenye hekima kuhusu ndoa. Walijitahidi sana kuboresha mawasiliano yao, kuhangaikiana, na kusameheana. (Methali 15:22; 1 Petro 3:7; 4:8) Walijifunza kuzuia hasira, na walimwomba Mungu awasaidie mambo yalipoharibika. (Wakolosai 3:19) Muda si muda, “Ukuta wa Berlin” uliporomoka!
-