Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Mathayo
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Januari 15
    • “UFALME WA MBINGUNI UMEKARIBIA”

      (Mt. 1:1–20:34)

      Kitabu cha Mathayo kinakazia suala la Ufalme na mafundisho ya Yesu, lakini hakifuati tarehe za matukio. Kwa mfano, Mahubiri ya Mlimani yanasimuliwa mwanzoni mwa kitabu hicho, ingawa Yesu aliyatoa karibu katikati ya huduma yake.

      Wakati wa huduma yake huko Galilaya, Yesu anafanya miujiza, anawapa wale mitume 12 maagizo kwa ajili ya huduma, anawashutumu Mafarisayo, na anatoa mifano kuhusu Ufalme. Kisha, anaondoka Galilaya na kuja “kwenye mipaka ya Yudea ng’ambo ya Yordani.” (Mt. 19:1) Akiwa njiani, Yesu anawaambia wanafunzi wake hivi: ‘Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa binadamu atahukumiwa kifo, na siku ya tatu atafufuliwa.’—Mt. 20:18, 19.

  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Mathayo
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Januari 15
    • “MWANA WA BINADAMU ATATOLEWA”

      (Mt. 21:1–28:20)

      Akiwa “amepanda juu ya punda,” Yesu anakuja Yerusalemu mnamo Nisani 9, 33 W.K. (Mt. 21:5) Kesho yake, anakuja hekaluni na kulisafisha. Katika Nisani 11, anafundisha hekaluni, anawashutumu waandishi na Mafarisayo, kisha anawapa wanafunzi wake “ishara ya kuwapo [kwake] na ya umalizio wa mfumo wa mambo.” (Mt. 24:3) Siku inayofuata, anawaambia hivi: “Mnajua kwamba siku mbili tangu sasa kutakuwa na pasaka, naye Mwana wa binadamu atatolewa ili atundikwe mtini.”—Mt. 26:1, 2.

      Ni Nisani 14. Baada ya kuanzisha Ukumbusho wa kifo chake, Yesu anasalitiwa, anakamatwa, anahukumiwa, na kutundikwa. Siku ya tatu, anafufuliwa kutoka kwa wafu. Kabla hajapanda kwenda mbinguni, Yesu aliyefufuliwa anawaamuru wafuasi wake hivi: “Kwa hiyo nendeni mkafanye wanafunzi kutoka kwa watu wa mataifa yote.”—Mt. 28:19.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki