-
Uhuru wa Kweli kwa WamayaMnara wa Mlinzi—2008 | Desemba 1
-
-
Hata hivyo, mambo ya kidini yalikuwa tofauti kabisa. Wamaya waliabudu miungu mingi; waliabudu miungu ya jua, mwezi, mvua, na mahindi, kati ya vitu vingine vingi. Viongozi wao wa kidini walichunguza nyota kwa makini. Ibada yao ilitia ndani matumizi ya uvumba, mifano, kujikata-kata, na mazoea ya kutoa wanadamu dhabihu, hasa wafungwa, watumwa, na watoto.
Wahispania Wawasili
Huo ndio utamaduni ambao Wahispania walipata mapema katika karne ya 16. Wavumbuzi Wahispania walikuwa na malengo mawili: kupata nchi mpya na utajiri na pia kuwageuza Wamaya wawe Wakatoliki ili kuwaweka huru kutokana na mazoea ya kipagani. Je, ushindi wa Wahispania uliwaletea Wamaya uhuru wa kweli, iwe ni wa kidini au kwa njia nyingine?
Wahispania, kutia ndani viongozi wa Kanisa Katoliki, walichukua ardhi ambayo Wamaya walikuwa wametumia tangu zamani kwa ajili ukulima uliohusisha kufyeka na kuchoma miti na majani ili kupanda mimea. Hilo lilisababisha hali ngumu sana na uhasama. Pia, wakoloni walidhibiti visima ambavyo vilikuwa chanzo pekee cha maji kwenye Rasi ya Yucatán. Hali ngumu hata zaidi zilitokea kanisa lilipoanza kutoza Wamaya kodi kila mwaka ya realea 12 1/2 kwa kila mwanamume na reale 9 kwa kila mwanamke. Kodi hiyo iliongezwa kwenye ile kodi ya kitaifa ambayo tayari ilikuwa imewalemea. Wahispania waliomiliki nchi walitumia vibaya hali hiyo kwa kuwalipia Wamaya kodi ya kanisa, kisha wakawalipisha deni hilo kwa kuwafanyisha kazi kama watumwa.
Pia, makasisi walitoza watu ada fulani kwa ajili ya huduma za kidini, kama vile ubatizo, ndoa, na mazishi. Kanisa lilijitajirisha huku Wamaya wakizidi kuwa maskini kwa sababu kanisa lilikuwa limenyakua ardhi yao, lilikuwa likiwatoza kodi, na ada. Wamaya walionwa kuwa washirikina na wapumbavu. Hivyo, makasisi na watawala wengine waliona kuwa ni jambo linalofaa kuwachapa Wamaya ili kuwafundisha adabu na kuwasaidia waache ushirikina.
-
-
Uhuru wa Kweli kwa WamayaMnara wa Mlinzi—2008 | Desemba 1
-
-
Hakuna Uhuru wa Kweli
Ukatoliki ulioletwa na Wahispania na vile vita kati ya Wahispania na Wamaya havikuleta uhuru wa kweli. Leo, kuna aina fulani ya dini inayounganisha utamaduni wa kabla ya enzi ya Wahispania na itikadi za Wakatoliki.
Kitabu kimoja (The Mayas—3000 Years of Civilization) kinasema hivi kuhusu Wamaya wa siku hizi: “Wamaya wanaabudu miungu yao ya zamani ya nguvu za asili na mababu wa kale kwenye mashamba, mapango, na milimani . . . na wakati uleule wanaabudu watakatifu kanisani.” Hivyo, mungu Quetzalcoatl, au Kukulcán analinganishwa na Yesu, na mungu wa kike wa mwezi analinganishwa na Bikira Maria. Isitoshe, badala ya kuabudu mti mtakatifu wa sufi wanaabudu msalaba na bado watu wanaunyunyizia maji kana kwamba ni mti halisi. Badala ya kuwa na mfano wa Yesu, misalaba ina maua ya msufi.
-