-
Michael Servetus—Alitafuta Ukweli Akiwa Peke YakeAmkeni!—2006 | Mei
-
-
Kutafuta Ukweli wa Kisayansi
Kwa kuwa alilazimika kuwakimbia watesaji wake, Servetus alibadili jina lake kuwa Villanovanus naye akaishi Paris, ambako alipata digrii ya sanaa na tiba. Udadisi wake wa mambo ya kisayansi ulimwongoza apasue miili ya wanadamu ili ajifunze jinsi inavyotenda kazi. Hivyo, yaelekea Servetus alikuwa Mzungu wa kwanza kufafanua mfumo wa mzunguko wa damu katika mapafu. Ufafanuzi wake umezungumziwa katika kitabu chake The Restitution of Christianity. Servetus alitoa maelezo hayo miaka 75 kabla ya William Harvey kufafanua mfumo kamili wa mzunguko wa damu.
-
-
Michael Servetus—Alitafuta Ukweli Akiwa Peke YakeAmkeni!—2006 | Mei
-
-
Pia Servetus aliandika kitabu Universal Treatise on Syrups chenye maoni yaliyosawazika kuhusu aina fulani ya matibabu. Ujuzi mwingi kuhusu matibabu unaopatikana katika kitabu hicho ulimfanya awe mtangulizi katika nyanja ya dawa na matumizi ya vitamini.
-
-
Michael Servetus—Alitafuta Ukweli Akiwa Peke YakeAmkeni!—2006 | Mei
-
-
[Picha katika ukurasa wa 20]
Servetus alichunguza mfumo wa mzunguko wa damu katika mapafu
[Hisani]
Anatomie descriptive et physiologique, Paris, 1866-7, L. Guérin, Editor
[Picha katika ukurasa wa 20]
Kitabu “Universal Treatise on Syrups” cha Servetus kilikuwa kitabu cha kwanza kutaja mambo fulani kuhusu dawa
-