-
Je, Sayansi Itamaliza Magonjwa?Amkeni!—2007 | Januari
-
-
◼ Nanomedicine Hiyo ni mbinu ya kitiba inayotumia nanotechnology, ambayo ni sayansi ya kutumia na kutokeza vitu vidogo sana. Kipimo kinachotumiwa katika teknolojia hiyo kinaitwa nanometa, ambayo ni sawa na sehemu moja ya bilioni ya meta.a
Ili kuelewa kipimo hicho, ukurasa huu unaosoma sasa una unene wa nanometa 100,000 hivi nao unywele wa mwanadamu una unene wa nanometa 80,000 hivi. Chembe nyekundu ya damu ina kipenyo cha nanometa 2,500. Bakteria ina urefu wa nanometa 1,000, na kirusi kina urefu wa nanometa 100. DNA yako ina kipenyo cha nanometa 2.5.
Watu wanaotetea teknolojia hii wanaamini kwamba karibuni wanasayansi watabuni vidude vidogo vinavyoweza kutumiwa wakati wa matibabu ndani ya mwili wa mwanadamu. Roboti hizo ndogo zitabeba kompyuta ndogo sana zilizo na maelekezo hususa. Kwa kushangaza, mashine hizo tata zitatengenezwa kwa kutumia vifaa vyenye ukubwa usiozidi nanometa 100. Hiyo ni ndogo mara 25 ukilinganisha na kipenyo cha chembe nyekundu ya damu!
Kwa sababu ni vidogo sana, inatarajiwa kwamba vifaa vya aina hiyo vitaweza kusafiri kwenye mishipa midogo sana na kupeleka oksijeni kwenye tishu zilizopungukiwa na damu, kuondoa vizuizi katika mishipa ya damu na kuondoa ukoga kwenye chembe za ubongo na hata kutafuta na kuharibu virusi, bakteria, na vitu vingine vinavyoambukiza magonjwa. Huenda mashine hizo zikatumiwa pia kupeleka dawa moja kwa moja kwenye chembe zilizokusudiwa.
Wanasayansi wanatabiri kwamba uwezo wa kugundua kansa utaongezeka kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya kutumia nanomedicine. Profesa wa kitiba, Dakt. Samuel Wickline alisema hivi: “Kuna uwezekano mkubwa sana wa kugundua kansa ndogo sana mapema na kuitibu kwa kutumia dawa zenye nguvu mahali palipoathiriwa, na wakati uleule kupunguza madhara ya dawa.”
Ingawa hilo linaweza kuonekana kuwa ndoto tu, wanasayansi fulani huona kwamba jambo hilo linawezekana. Wale wanaoongoza uchunguzi huo wanatarajia kwamba katika miaka kumi ijayo nanotechnology itatumiwa katika kurekebisha na kupanga upya muundo wa molekuli katika chembe za uhai. Mtetezi mmoja wa teknolojia hiyo anadai: “Nanomedicine hatimaye itaondoa magonjwa yote ya karne ya 20, itaondoa maumivu na kuteseka kote kunakotokana na matibabu, na kuwawezesha wanadamu kupanua uwezo wao.” Hata sasa wanasayansi wanapata matokeo mazuri wanapotumia nanomedicine kwa wanyama walio kwenye maabara.
-
-
Je, Sayansi Itamaliza Magonjwa?Amkeni!—2007 | Januari
-
-
a Neno “nano” linatokana na neno la Kigiriki mbilikimo linalomaanisha “sehemu moja ya bilioni.”
-
-
Je, Sayansi Itamaliza Magonjwa?Amkeni!—2007 | Januari
-
-
Nanomedicine
Mashine ndogo sana ambazo huenda zitawasaidia madaktari kutibu magonjwa ndani ya chembe. Picha inaonyesha wazo la mchoraji la “nanomachine,” yaani, roboti ndogo sana ambazo zinaweza kuiga utendaji wa chembe nyekundu za damu
[Hisani]
Artist: Vik Olliver (vik@diamondage.co.nz)/Designer: Robert Freitas
-