-
Kuuchunguza Mwili Bila Kufanya UpasuajiAmkeni!—2008 | Novemba
-
-
Positron-Emission Tomography
Inafanyaje kazi? Ili mtu achunguzwe kupitia PET scan, umaji-maji wenye mnururisho huchanganywa na kemikali inayopatikana mwilini, hasa glukosi na kutiwa mwilini. Positron zinapotokezwa katika tishu picha huweza kupigwa. Chembe zenye kansa hutumia glukosi nyingi kuliko chembe za kawaida, hivyo zinavuta umaji-maji wenye mnururisho. Kwa sababu hiyo, tishu zilizoathiriwa hutokeza positron nyingi zaidi ambazo huonekana kwa rangi mbalimbali katika picha.
Ingawa CT scan na MRI scan huonyesha umbo na muundo wa viungo na tishu, PET scan zinaonyesha jinsi zinavyofanya kazi, na hivyo kuonyesha mabadiliko mapema zaidi. PET scan zinaweza kufanywa pamoja na CT scan, na hivyo kutokeza picha yenye mambo mengi zaidi. Hata hivyo, PET scan zinaweza kutokeza picha zisizo sahihi ikiwa mgonjwa alikula muda fulani kabla ya kupigwa eksirei hiyo au ikiwa kiwango cha sukari kwenye damu kimepanda, pengine kwa sababu ya kisukari. Pia, kwa sababu umaji-maji huo wenye mnururisho unaisha nguvu haraka, ni muhimu picha hiyo ipigwe haraka.
Madhara: Kwa kuwa umaji-maji unaotumiwa una kiasi kidogo cha mnururisho unaoisha nguvu haraka, hauathiri mtu sana. Lakini bado unaweza kuhatarisha kijusi. Kwa sababu hiyo, wanawake ambao ni wajawazito wanapaswa kuwafahamisha madaktari na wale wanaopiga eksirei. Wanawake ambao hawajapita umri wa kuzaa wanaweza kuomba wapimwe damu au mkojo ili kuchunguza ikiwa ni wajawazito. Ikiwa PET scan inatumiwa pamoja na CT scan, mtu anapaswa kufikiria madhara yanayotokana na CT scan.
Faida: Kwa sababu PET scan hazionyeshi tu umbo la viungo na tishu bali pia jinsi zinavyofanya kazi, eksirei hizo zinaweza kutambua matatizo kabla ya mabadiliko katika muundo wa tishu kuonekana kupitia eksirei ya CT au MRI.
-
-
Kuuchunguza Mwili Bila Kufanya UpasuajiAmkeni!—2008 | Novemba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 12]
PET
[Hisani]
Courtesy Alzheimer’s Disease Education and Referral Center, a service of the National Institute on Aging
-