-
Tauni Mbaya Zaidi Katika HistoriaAmkeni!—2005 | Desemba 22
-
-
Sayansi Iliposhindwa
Kufikia mwanzoni mwa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu, ilionekana kwamba sayansi ya tiba ilikuwa imefanya maendeleo makubwa kushinda magonjwa. Hata wakati wa vita hivyo, madaktari walijivunia mafanikio waliyopata katika kupunguza athari za magonjwa ya kuambukiza. Wakati huo, jarida The Ladies Home Journal lilisema kwamba Wamarekani hawakuhitaji tena kuwa na vyumba vya kuwalaza waliokufa ili kuwatazama. Lilidokeza kwamba kuanzia wakati huo vyumba hivyo viitwe vyumba vya walio hai. Lakini homa ya Hispania ikalipuka, nayo sayansi ya tiba ikashindwa kabisa.
Crosby anaandika: “Madaktari wote wa 1918 walichangia kushindwa kabisa kwa sayansi ya tiba katika karne ya 20 au, ikiwa kushindwa kwa tiba kungetegemea idadi ya vifo, basi madaktari hao walichangia kushindwa kabisa kwa sayansi ya tiba katika historia yote.” Ili madaktari peke yao wasilaumiwe, Barry anatoa hoja hii: “Wakati huo wanasayansi walielewa kabisa ukubwa wa tisho hilo, walijua jinsi ya kutibu aina nyingi za bakteria zinazosababisha nimonia, nao walitoa mashauri ya afya kwa umma ambayo yangeokoa makumi ya maelfu ya Wamarekani. Wanasiasa walipuuza mashauri hayo.”
-
-
Mambo Tunayojua Sasa Kuhusu HomaAmkeni!—2005 | Desemba 22
-
-
Mambo Tunayojua Sasa Kuhusu Homa
NI MWAKA wa 1997. Mwanasayansi ameketi katika kijiji kidogo cha Waeskimo cha Brevig kwenye nyika yenye barafu ya Peninsula ya Seward huko Alaska. Mbele yake kuna mwili wa mwanamke kijana ambaye mwanasayansi huyo na Waeskimo wanne walifukua kutoka kwenye barafu. Alikufa kwa homa mwaka wa 1918 na mwili wake ulioganda umekuwa mahali hapo tangu wakati huo.
Kuna manufaa gani ya kuchunguza mwili wake sasa? Wanasayansi wanatumaini kwamba kitu kilichosababisha homa hiyo kingali mapafuni mwake na kwamba kwa kutumia mbinu ya hali ya juu ya kuchunguza chembe za urithi wataweza kukitenga, kukichunguza, na kukitambulisha. Kwa nini ujuzi huo utakuwa wenye manufaa? Ili kujibu swali hilo, tunahitaji kuelewa vizuri zaidi jinsi ambavyo virusi hufanya kazi na ni nini hufanya viwe hatari sana.
Virusi Vinavyoweza Kuwa Hatari
Leo tunajua kwamba homa husababishwa na virusi na kwamba inaweza kuenezwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kukohoa, kupiga chafya, na kuzungumza. Homa iko kila mahali ulimwenguni hata katika nchi za Tropiki, ambako inaweza kutokea mwaka mzima. Katika nchi zilizo kaskazini mwa ikweta, msimu wa homa huanza Novemba hadi Machi; na katika nchi zilizo kusini mwa ikweta, msimu huo huanza Aprili hadi Septemba.
Virusi aina ya A vinavyosababisha homa ambavyo ndivyo hatari zaidi, ni vidogo vinapolinganishwa na virusi vingi. Kwa kawaida vina umbo la mviringo na vina vitu fulani vilivyochomoza. Virusi hivyo vinaposhambulia chembe ya mwanadamu, huzaana haraka sana hivi kwamba kwa muda wa saa kumi hivi, kati ya “nakala” mpya 100,000 na milioni moja za virusi vya homa hulipuka kutoka kwenye chembe hiyo.
Jambo linaloogopesha kuhusu virusi hivyo ni kwamba vinaweza kubadilika haraka. Kwa kuwa virusi hivyo huzaana haraka sana (haraka zaidi kuliko virusi vya HIV), “nakala” zake nyingi hazifanani kabisa. Nyingine ni tofauti sana hivi kwamba hazitambuliwi na mfumo wa kinga. Kwa sababu hiyo, kila mwaka sisi hushambuliwa na virusi tofauti vya homa vyenye antijeni tofauti na hilo hufanya iwe vigumu kwa mfumo wetu wa kinga kuvitambua na kuvishambulia. Ikiwa antijeni hizo zitabadilika mara nyingi, mfumo wetu wa kinga hautakuwa na uwezo wa kujikinga na kuna hatari ya homa hiyo kuenea ulimwenguni pote.
Isitoshe, wanyama pia huambukizwa virusi vya homa na jambo hilo hutokeza tatizo kwa wanadamu. Inaaminika kwamba nguruwe huwa na virusi ambavyo huambukizwa ndege kama vile kuku na mabata. Lakini anaweza pia kuwa na virusi vingine vinavyoambukizwa wanadamu.
Kwa hiyo, nguruwe akiambukizwa aina mbili za virusi, yaani virusi vinavyoambukizwa wanyama na vile vinavyoambukizwa wanadamu, chembe za urithi za virusi hivyo zinaweza kuchanganyika. Hilo linaweza kutokeza virusi vipya vya homa visivyo na kinga. Watu fulani hufikiri kwamba wakulima ambao hufuga kuku na nguruwe, kama huko barani Asia, wanaweza kuambukizwa virusi vipya vya homa.
Kwa Nini Homa Hiyo Ilienea Sana?
Swali ni, Ni nini kilichosababisha virusi vya homa ya 1918-1919 vigeuke na kuwa virusi vilivyosababisha nimonia iliyoua vijana wengi sana? Ingawa virusi hivyo havipo tena, kwa muda mrefu wanasayansi wamehisi kwamba ikiwa wangeweza kupata virusi hivyo vikiwa vimegandishwa, wangeweza kutenganisha RNA zake zikiwa nzima na kugundua kilichofanya ziwe hatari hivyo. Kwa kweli, kwa kiwango fulani wamefaulu kufanya hivyo.
Mwili ulioganda ambao ulipatikana huko Alaska, uliotajwa mwanzoni mwa makala hii, umesaidia kikundi cha wanasayansi kutambua na kuona muungano wa chembe za urithi za virusi vilivyosababisha homa ya 1918-1919. Hata hivyo, bado wanasayansi hawajagundua ni nini kilichofanya homa hiyo iue watu wengi sana. Inaonekana kwamba virusi hivyo vinafanana na virusi vya homa ambavyo huambukiza nguruwe na ndege.
-