-
Kuuchunguza Mwili Bila Kufanya UpasuajiAmkeni!—2008 | Novemba
-
-
Eksirei
Inafanyaje kazi? Eksirei zina mawimbi mafupi kuliko yale ya mwangaza kwa hiyo, zinaweza kupenya tishu za mwili. Sehemu fulani ya mwili inapopigwa eksirei, tishu ngumu, kama vile, mifupa, hufyonza miale na kuwa na rangi nyangavu kwenye eksirei. Tishu nyepesi huonekana zikiwa na rangi ya kijivu. Mara nyingi eksirei hutumiwa kutambua matatizo au magonjwa ya meno, mifupa, matiti, na kifua. Ili kutofautisha kati ya tishu nyepesi zenye upana uleule, daktari anaweza kumdunga mgonjwa sindano yenye umaji-maji wa rangi fulani usiopenya miale ili kuonyesha tofauti. Siku hizi, eksirei huonekana kupitia kompyuta.
Madhara: Kuna uwezekano wa chembe na tishu kuharibiwa, lakini kwa kawaida madhara ni machache yakilinganishwa na faida.b Kabla ya kufanyiwa eksirei, wanawake wanapaswa kuwafahamisha madaktari wao ikiwa wao ni wajawazito. Pia huenda mtu akaathiriwa na rangi za kutofautisha tishu kama vile iodini. Hivyo, mwambie daktari au mtaalamu wako ikiwa unaathiriwa na iodini au chakula cha baharini ambacho huwa na iodini.
Faida: Picha za eksirei zinatokezwa haraka, kwa kawaida hazina maumivu, ni za bei rahisi, na zinapigwa kwa urahisi. Hivyo, zinafaa hasa kutumiwa kuchunguza matiti na matatizo ya dharura. Hakuna mnururisho unaobaki mwilini baada ya eksirei kupigwa, na hivyo kwa kawaida hakuna madhara.c
-
-
Kuuchunguza Mwili Bila Kufanya UpasuajiAmkeni!—2008 | Novemba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 11]
Eksirei
-