Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Kambodia

      Painia mmoja huko Kambodia anayeitwa Louy, husafiri kwa baiskeli kwenda kijiji kimoja ambako huongoza mafunzo ya Biblia. Siku tatu kabla ya Ukumbusho, alipokuwa katika kijiji hicho, akizungumza na mmoja kati ya wanafunzi wake kuhusu Ukumbusho, watoto walianza kukusanyika na kumuuliza maswali. Idadi ya watoto hao ilizidi kuongezeka. Louy akawapa mialiko 57. Siku iliyofuata Louy alipanda baiskeli yake na kwenda mpaka kijijini kuongoza funzo lingine la Biblia. Mwanafunzi huyo alimwambia kwamba ndugu zake na marafiki pia wangependa kuhudhuria. Louy akampa mialiko 20 awape. Louy alianza kujiuliza atawasaidia jinsi gani watu wote hao kufika kwenye Ukumbusho. Baada ya kusali, alizungumza na baba ya mmoja kati ya mafunzo yake, ambaye ni mzee wa kijiji. Baba huyo akamhakikishia Louy kwamba ikiwa atapata tuk-tuk au bajaji, kila mmoja anaweza kwenda. Wanaweza kusimama au kupakatana. Louy alifurahi sana watu 18 walipohudhuria kutoka kijiji hicho.

  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 55]

      Alikodisha tuk-tuk (bajaji) moja

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki