Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • KUADHIMISHA UKUMBUSHO

      Kila mwaka, akina ndugu walijaribu kuadhimisha Ukumbusho kambini. Miaka yote waliyokuwa katika kambi moja huko Mordvinia, hakuna ndugu aliyekosa tukio hilo. Bila shaka, wasimamizi wa kambi walijaribu kulizuia. Walijua tarehe ya Ukumbusho, na kwa kawaida waliwaambia walinzi wote wawe macho. Hata hivyo, walinzi wengi walichoka kuwachunguza akina ndugu ilipofika jioni kwa sababu hakuna aliyejua wakati na mahali ambapo Ukumbusho ungefanywa.

      Akina ndugu walijitahidi kupata divai na mkate usiotiwa chachu. Wakati mmoja walinzi waligundua mifano hiyo kwenye droo siku ya Ukumbusho na wakaichukua. Baadaye, kikundi hicho kilibadilishwa, na ndugu aliyekuwa akisafisha ofisi ya kamanda alichukua mifano hiyo na kuwapa akina ndugu bila kuonekana. Jioni hiyo ndugu waliadhimisha Ukumbusho wakiwa na mifano wakati wa zamu ya kikundi cha tatu. Mifano hiyo ilihitajika sana kwani ndugu mmoja alikuwa mtiwa mafuta.

      KUADHIMISHA UKUMBUSHO KATIKA KAMBI YA WANAWAKE

      Kambi nyingine zilikuwa na tatizo hilohilo. Valentina Garnovskaya anakumbuka ilivyokuwa vigumu kuadhimisha Ukumbusho katika kambi ya wanawake huko Kemerovo. Anasema: “Kambi hiyo ilikuwa na dada 180. Tulikatazwa kukutana. Kwa miaka kumi tulifaulu kuadhimisha Ukumbusho mara mbili tu. Wakati mmoja tuliamua kuadhimisha Ukumbusho katika ofisi niliyopaswa kusafisha. Akina dada walianza kuingia ofisini bila kuonekana kwa muda wa saa kadhaa kabla ya Ukumbusho. Dada 80 hivi walifika. Tuliweka mkate usiotiwa chachu na divai nyekundu mezani.

      “Tuliamua kuanza bila kuimba, hivyo dada mmoja akatoa sala ya kufungua, na tukaanza kwa shangwe na kwa njia inayofaa. Lakini ghafula tulisikia kelele na tukagundua kuwa wanyapara walikuwa wakitutafuta. Kisha tukaona msimamizi wao akichungulia dirishani, ingawa dirisha hilo lilikuwa juu sana. Mlango ulibishwa kwa nguvu na wakatuamuru tuufungue. Wanyapara waliingia kwa kishindo na kumkamata dada aliyekuwa akitoa hotuba na kumpeleka katika kifungo cha upweke. Kwa ujasiri dada mwingine alisimama atoe hotuba hiyo, lakini wakamkamata pia. Alipochukuliwa, dada mwingine akajaribu kuendelea na hotuba hiyo, kwa hiyo wakatukusanya katika chumba kingine, wakitisha kutuadhibu kwa kifungo cha upweke. Hapo ndipo tulipomaliza mwadhimisho wa Ukumbusho kwa wimbo na kufunga kwa sala.

      “Tuliporudi mahali pa kulala, wafungwa wengine walituambia, ‘Mlipotoweka ghafula, tulisema Har–Magedoni imekuja na Mungu amewachukua na kuwapeleka mbinguni akituacha hapa tuangamie!’ Tulikuwa na wafungwa hao kwa miaka kadhaa na hawakuwa wamekubali kweli. Lakini baada ya hapo, baadhi yao walianza kutusikiliza.”

  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 184, 185]

      Miaka yote waliyokuwa katika kambi moja huko Mordvinia, hakuna ndugu aliyekosa Ukumbusho

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki