Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matukio Muhimu Ya Mwaka Uliopita
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ndugu nchini Mexico waliwaalika mafundi wa kampuni ya MAN kwenye Ukumbusho. Wanne walikubali kuhudhuria, lakini hawakuwa na mavazi yanayofaa. Hivyo, Mwanabetheli fulani akawapeleka madukani kwa sababu walitaka kununua suti. Ndugu waliwapa Biblia na wakati wa hotuba ya Ukumbusho wakawasaidia kufungua maandiko. Baada ya mkutano, mafundi hao walipiga picha na kutabasamu sana hivi kwamba wengi kutanikoni walifikiri wao ni Wanabetheli kutoka Ujerumani.

  • Matukio Muhimu Ya Mwaka Uliopita
    2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Huko Mexico mtu aliyeleta vifereji vya kuwekwa kwenye matbaa mpya alishangazwa na utulivu alioona kwenye ofisi ya tawi. Aliuliza maswali mengi, na sasa yeye na familia yake wanajifunza Biblia na wanafanya maendeleo. Msimamizi wa wajenzi fulani wenyeji aliomba jambo lisilo la kawaida. Alisema: “Kwa kawaida watu hutupa bakshishi ili kutushukuru kwa kazi yetu. Mwaonaje mkitupa sisi sote Biblia badala ya bakshishi? Kutokana na mambo niliyoona hapa, ninafikiri kwamba kuijua Biblia ni muhimu zaidi kuliko pesa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki