Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Shetani Ni Hadithi Tu au Ni Mtu Halisi Mwovu?
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 15
    • Kule kuamini kwamba watu wanaweza kupagawa na Ibilisi au roho waovu kulifanya watu waogope sana mambo ya uchawi. Tokea karne ya 13 hadi 17, kotekote Ulaya watu wakaogopa sana wachawi na woga huo ukasambazwa hata Amerika Kaskazini na watu waliotoka Ulaya. Hata watetezi Waprotestanti wa marekebisho ya kidini kama Martin Luther na John Calvin waliidhinisha tabia ya kuwasaka wachawi. Kule Ulaya, mashtaka yaliyotegemea uvumi tu au shutuma zisizo za kweli yalisikilizwa na Mabaraza ya Kuhukumu Wazushi au na mahakama za nchi. Kwa kawaida watu walikuwa wakiteswa ili wakubali “hatia.”

      Wale waliopatikana na hatia wangeweza kuhukumiwa kifo kwa kuteketezwa moto, na katika Uingereza na Scotland, hukumu hiyo ingetekelezwa kwa kunyongwa. Kitabu The World Book Encyclopedia kinasema hivi kuhusu idadi ya wale waliohukumiwa: “Kulingana na baadhi ya wanahistoria, tokea mwaka wa 1484 hadi 1782, kanisa la Kikristo liliwaua wanawake wapatao 300,000 kwa kuwashuku kuwa wachawi.” Ikiwa Shetani ndiye aliyechochea ukatili huo, basi alitumia nani kutekeleza mauaji hayo? Je, ni wale waliouawa au aliwatumia wanyanyasi shupavu wa kidini?

  • Je, Shetani Ni Hadithi Tu au Ni Mtu Halisi Mwovu?
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 15
    • [Picha katika ukurasa wa 6]

      Kuhofu wachawi kulizusha mauaji ya mamia ya maelfu ya watu

      [Hisani]

      From the book Bildersaal deutscher Geschichte

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki