Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Fulizeni Kunitarajia”
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
    • Kwa habari ya Moabu na Amoni, kulingana na Yosefo, mwanahistoria Myahudi, katika mwaka wa tano baada ya Yerusalemu kuanguka, Wababiloni walipiga vita nao na kuwashinda. Wao nao walipotelea mbali, kama ilivyotabiriwa.

  • “Fulizeni Kunitarajia”
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
    • “Mimi nimeyasikia matukano ya Moabu, na dhihaka za wana wa Amoni, ambazo kwa hizo wamewatukana watu wangu, na kujitukuza juu ya mpaka wao. Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima

  • “Fulizeni Kunitarajia”
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
    • 14. Kuna uthibitisho gani kwamba mataifa ya kigeni ‘yalijitukuza’ juu ya Waisraeli na Mungu wao, Yehova?

      14 Moabu na Amoni walikuwa maadui wa Israeli wa tangu zamani. (Linganisha Waamuzi 3:12-14.) Jiwe la Moabu, lililo katika Louvre Museum katika Paris, lina maandiko yenye taarifa ya kujisifu iliyotolewa na Mfalme Mesha wa Moabu. Yeye asimulia kwa majivuno jinsi alivyotwaa majiji kadhaa ya Israeli kwa msaada wa mungu wake Kemoshi. (2 Wafalme 1:1)

  • “Fulizeni Kunitarajia”
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Machi 1
    • 15. Yehova angeaibishaje miungu ya mataifa yaliyojitukuza juu ya watu wake?

      15 Zaburi 83 hutaja mataifa kadhaa, kutia ndani Moabu, Amoni, na Ashuru, waliojitukuza juu ya Israeli, na kusema hivi kwa kujigamba: “Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa, na jina la Israeli halitakumbukwa tena.” (Zaburi 83:4) Nabii Sefania alitangaza kwa moyo mkuu kwamba mataifa hayo yote yenye kiburi na miungu yayo yangeaibishwa na Yehova wa majeshi. “Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa BWANA wa majeshi, na kujitukuza juu yao. BWANA atakuwa mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawafisha kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.”—Sefania 2:10, 11.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki