-
Kutumia Kileo Vibaya—Kunaathiri AfyaAmkeni!—2005 | Oktoba 8
-
-
Kiasi Kisichodhuru
Kuna matatizo mengine ya afya mbali na yale yaliyotajwa. Mnamo 2004, makala moja katika gazeti Nature ilisema kwamba “hata kiasi kidogo cha kileo huzidisha hatari ya kujeruhiwa na huongeza uwezekano wa kupatwa na magonjwa 60 hivi.” Kwa hiyo, ni kiasi gani ambacho hakidhuru? Leo mamilioni ya watu ulimwenguni hunywa kileo mara mojamoja. Ili kuwa na afya bora ni vizuri kuwa na kiasi. Lakini kiasi ni nini? Huenda watu wengi wakaona kwamba kiasi wanachotumia ni cha kadiri, labda wakifikiri kwamba maadamu hawalewi au wao si waraibu, hakuna tatizo. Hata hivyo, mwanamume 1 kati ya 4 barani Ulaya hutumia kiasi cha kileo ambacho huonwa kuwa hatari.
Ripoti mbalimbali hufafanua kunywa kwa kiasi kuwa kunywa gramu 20 za kileo kikali kwa siku, au pombe mbili za kawaida kwa wanaume, na gramu 10, yaani, pombe moja kwa wanawake. Wizara ya afya ya Ufaransa na Uingereza inadokeza “kiwango kinachofaa” kuwa pombe tatu kwa siku kwa wanaume na mbili kwa wanawake. Taasisi ya Marekani Inayoshughulikia Matumizi Mabaya ya Kileo na Uraibu pia inapendekeza “watu wenye umri wa miaka 65 na zaidi wapunguze kileo na kunywa pombe moja kwa siku.”c Hata hivyo, sote huathiriwa na kileo kwa njia tofauti. Watu fulani wanaweza kulemewa na viwango hivyo vidogo. Kwa mfano, Ripoti Maalumu ya 10 ya Bunge la Marekani Kuhusu Kileo na Afya, inasema, “kiasi kinachofaa cha kileo kinaweza kuwadhuru watu wenye wasiwasi na matatizo ya kihisia.” Watu wanapaswa kuzingatia umri, hali ya afya, na maumbile.—Ona sanduku “Kupunguza Hatari.”
-
-
Kutumia Kileo Vibaya—Kunaathiri AfyaAmkeni!—2005 | Oktoba 8
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 8]
KUPUNGUZA HATARI
Maelezo yafuatayo yanayofafanua jinsi ya kupunguza hatari yalichapishwa na Idara ya Magonjwa ya Akili na Uraibu wa Madawa ya Kulevya ya Shirika la Afya Ulimwenguni. Maelezo hayo ya kupunguza hatari hayamaanishi kwamba mtu hawezi kupatwa na madhara yoyote kwa kutumia kileo. Watu huathiriwa na kileo kwa njia tofauti.
◼ Usinywe zaidi ya vipimo viwili vya kawaida kwa sikue
◼ Usinywe kileo angalau siku mbili kwa juma
Unapokuwa katika hali zifuatazo, hata chupa moja au mbili zinaweza kupita kiasi:
◼ Unapoendesha gari au kutumia mashini
◼ Unapokuwa mjamzito au unaponyonyesha
◼ Unapotumia dawa fulani
◼ Unapokuwa na matatizo fulani ya afya
◼ Ikiwa huwezi kudhibiti kunywa kileo
[Maelezo ya Chini]
e Kipimo cha kawaida ni sawa na gramu 10 ya kileo kwa kila glasi moja.
[Hisani]
Chanzo: Brief Intervention for Hazardous and Harmful Drinking
-