Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Moldova
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • Jitihada za Kuhalalisha Kazi ya Kuhubiri

      Baada ya kazi ya kuhubiri kupigwa marufuku mwaka wa 1925, ndugu kwenye ofisi ya Cluj-Napoca, Rumania, walituma ripoti yenye kurasa 50 kwa waziri wa madhehebu. Ripoti hiyo ilikuwa na maelezo mafupi kuhusu imani na mafundisho yetu, na pia ilitia ndani ombi rasmi la kuondoa marufuku. Hivyo, mnamo Septemba 1927, ndugu mmoja aliruhusiwa kumwona waziri huyo mara tatu. Baada ya kumwona waziri kwa mara ya tatu alitumaini kwamba sheria ingebadilishwa na Mashahidi wangepata uhuru wa ibada. Kwa kusikitisha, serikali ilipuuza maombi ya ndugu huyo. Hali ilizidi kuwa mbaya kwa watu wa Yehova kwa kuwa maafisa waliendelea kutunga matatizo kwa njia ya amri. (Zab. 94:20; Dan. 6:5-9) Hati rasmi iliyotolewa Mei 29, 1932, ilisema kwamba “utendaji wote” wa Wanafunzi wa Biblia “umepigwa marufuku kabisa.”

  • Moldova
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • Mei 6, 1937, ndugu katika wilaya iyo hiyo walimwandikia hakimu mkuu na kumwomba aifute dini ya Mashahidi wa Yehova kutoka katika orodha ya madhehebu yasiyo halali. Jibu rasmi kutoka kwa wenye mamlaka lilionyeshwa katika barua ambayo meya wa wilaya ya Soroca alimwandikia hakimu mkuu wa wilaya hiyo. Barua hiyo iliyoandikwa Juni 15, 1937, ilisema hivi: “Utendaji wa [Mashahidi wa Yehova] umepigwa marufuku na . . . Wizara ya Madhehebu na Sanaa. Kwa hiyo, hatuwezi kukubali ombi lao la kufuta dini ya Mashahidi wa Yehova kutoka katika orodha ya madhehebu yasiyo [halali], kwa kuwa wao wanaendeleza dini hiyo.”

      Jarida rasmi la serikali la Monitorul Oficial, la Julai 12, 1939, lilionyesha uhasama huo kwa kusema kwamba Mashahidi wa Yehova na mashirika yote wanayotumia “yamepigwa marufuku kabisa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki