Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Moldova
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • Kati yao kulikuwa na Mashahidi kadhaa kutia ndani Nicolae Anischevici. Nicolae anasema hivi: “Walipokuwa wakituandikisha, polisi walituamuru tushiriki katika sherehe fulani ya kidini. Sisi Mashahidi tulikataa. Tulikataa pia kubeba silaha. Kwa hiyo, polisi walitushutumu kuwa Wakomunisti na wakatukamata. Hata hivyo kabla ya kutufunga, walituruhusu kueleza sababu ya kutojiunga na jeshi.

      “Kesho yake tulihamishwa hadi Briceni, kitovu cha mahakama ya wilaya hiyo. Tulivuliwa mavazi yote na miili yetu ikachunguzwa kabisa. Kisha kasisi mwenye cheo cha juu jeshini akatuhoji. Alikuwa mwenye fadhili, alielewa kwamba uamuzi wetu ulitegemea dhamiri, na alipanga tupewe chakula. Na zaidi ya hayo, aliandika kwamba tulikataa kujiunga na jeshi kwa sababu tunamwamini Yesu.

      “Kutoka Briceni tulipelekwa hadi kwenye kituo cha polisi huko Lipcani. Huko, polisi walitupiga kikatili hadi usiku. Kisha wakatufunga katika chumba fulani pamoja na ndugu wengine wawili na mwanamke mmoja. Baadaye tuligundua kwamba mwanamke huyo alikuwa mpelelezi. Tulipigwa kila siku, kwa siku kadhaa. Hatimaye, mimi nilipelekwa Chernovtsy ili nihukumiwe katika mahakama ya jeshi. Nilipewa wakili ambaye alinisaidia sana nikiwa huko. Hata hivyo, afya yangu ilikuwa imezorota sana kwa sababu ya mateso hivi kwamba wakuu wa jeshi walifikiri ningekufa. Mwishowe waliamua kunipeleka nyumbani bila kunihukumu.”

  • Moldova
    2004 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
    • [Picha katika ukurasa wa 94]

      Nicolae Anischevici

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki