Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Maadili Ni Mabaya Zaidi Kuliko Awali?
    Amkeni!—2000 | Aprili 8
    • Kwanza, katika miaka ya karibuni watoto na matineja wengi zaidi wamefanya vitendo vikatili vya jeuri dhidi ya watoto wengine na vilevile dhidi ya watu wazima.

      Kisa chenye kushtua kilitukia huko Sweden mwaka wa 1998. Wavulana wawili, wenye umri wa miaka mitano na saba, walimkaba koo mwenzao mwenye umri wa miaka minne waliyekuwa wakicheza naye hadi akafa! Wengi walijiuliza swali hili: Je, watoto hawana uwezo wa kujizuia kabla ya kufanya jambo linalopita kiasi? Daktari wa magonjwa ya akili ya watoto alitoa maelezo haya yenye uzito: “Kujizuia kufanya jambo linalopita kiasi, ni jambo ambalo lazima watu wajifunze,” alisema. “Kungehusu . . . vielelezo ambavyo watoto huona na kile wanachojifunza kutoka kwa watu wazima walio karibu nao.”

  • Je, Maadili Ni Mabaya Zaidi Kuliko Awali?
    Amkeni!—2000 | Aprili 8
    • Hata miongoni mwa watoto na vijana wanaoonekana kuwa wa kawaida, watazamaji wameona maadili yakipuuzwa. “Tumerudia maadili ya Enzi ya Vyombo vya Mawe,” adai Christina Hoff Sommers, profesa wa falsafa. Alisema kwamba wanafunzi wake wachanga wanapokabili suala lihusulo jambo linalofaa na lisilofaa, wengi wao hawajihisi salama kabisa. Kisha hujibu kwamba hakuna kitu kama jambo linalofaa au lisilofaa. Wanaamini kwamba kila mtu apaswa kufikiria kile kinachomfaa.

      Katika nyakati za karibuni, wengi wa wanafunzi wake wamepinga kanuni ya adhama ya pekee na thamani ya uhai wa kibinadamu. Kwa mfano, walipoulizwa wangefanya nini ikiwa wangekabili uamuzi kati ya kuokoa uhai wa mnyama kipenzi wao au uhai wa mwanadamu mwenzao wasiyemjua, wengi walisema wangechagua mnyama huyo.

      “Tatizo si kwamba vijana hawana ujuzi, hawaaminiki, ni wakatili, au ni wahaini,” asema Profesa Sommers. “Kusema waziwazi, hawajui jema na baya.” Adai kwamba vijana wengi leo kwa kweli hutilia shaka kama kuna jema au baya, anaona kwamba mtazamo huo hutokeza mojawapo ya tisho kubwa zaidi kwa jamii.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki