Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Magonjwa Yanayoenezwa na Wadudu Yanaongezeka
    Amkeni!—2003 | Mei 22
    • Kwa mfano, ingawa kuna maelfu ya aina za mbu, aina moja tu ya mbu anayeitwa Anopheles ndiye anayeeneza viini vya malaria. Ugonjwa huo huua watu wengi zaidi kati ya magonjwa yote ya kuambukizwa duniani (baada ya kifua kikuu).

      Hata hivyo, aina nyingine za mbu hueneza magonjwa mengine mengi. Shirika la Afya Ulimwenguni laripoti hivi: “Kati ya wadudu wanaoeneza magonjwa, mbu ndio hatari zaidi kwa sababu wao hueneza malaria, kidingapopo, na homa ya manjano, magonjwa ambayo huua watu milioni kadhaa na kuwapata mamia ya mamilioni ya watu kila mwaka.” Angalau asilimia 40 ya watu duniani wamo katika hatari ya kuambukizwa malaria, na asilimia 40 hivi wamo katika hatari ya kupata ugonjwa wa kidingapopo. Katika sehemu nyingi, watu huambukizwa yote mawili.

  • Kwa Nini Yamerudi?
    Amkeni!—2003 | Mei 22
    • Lakini joto linaweza pia kusababisha hali nyinginezo. Katika maeneo fulani yenye joto, mito hukauka na kuwa vidimbwi, na katika maeneo mengine joto husababisha mvua na mafuriko ambayo hutokeza vidimbwi vyenye maji yaliyotuama. Mbu huzaana katika maji hayo. Joto hufanya mbu wazaane haraka, na kuwafanya wadumu kwa muda mrefu. Mbu huwa watendaji sana kunapokuwa na joto. Joto hilo huingia katika utumbo wao na kufanya viini vilivyomo vizaane haraka. Hivyo, mbu akimuuma mtu mara moja wakati wa joto, kuna uwezekano mkubwa kwamba mtu huyo ataambukizwa ugonjwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki