Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Msumbiji

      Mnamo 1992, Madalena alihusika katika aksidenti iliyomlemaza alipokuwa na umri wa miaka 30 hivi. Baada ya aksidenti hiyo, haikuwa rahisi kutoka nyumbani. Miaka mitatu baadaye, Mashahidi walizungumza na baba yake nje ya nyumba yao. Baba yake alikuwa kiongozi wa kikundi fulani cha dini ya kienyeji kilichokutana nyuma ya nyumba yake. Madalena aliyekuwa akisikiliza mazungumzo hayo, aliwasikia ndugu hao wakiuliza habari zake, ndipo akawaalika ndani ya nyumba. Aliguswa moyo sana alipotambua walimjali kikweli! Alikubali kujifunza Biblia na akapendezwa sana na mambo aliyojifunza. Walipoona bidii yake, Mashahidi walimsaidia kwa njia mbalimbali, na hata kumsaidia kufika kwenye mikutano. Kwa sababu ya msaada huo, Madalena alijiweka wakfu kwa Yehova na kubatizwa mwaka wa 2002.

      Wazazi wa Madalena walivutiwa sana na jinsi Mashahidi walivyomtunza binti yao. Mama yake alianza kuhudhuria mikutano na akaacha dini ya mume wake. Mwanzoni, babake Madalena alisema hataiacha dini yake, lakini baada ya muda yeye pia akaanza kuhudhuria mikutano. Watu wa dini yake walimshinikiza aache kwenda mikutanoni kwa sababu alikuwa kiongozi wao. Hata hivyo, alisimama imara na kuteketeza vitu vyake vya kidini. Yeye na mke wake walibatizwa mwaka wa 2007. Familia nzima inafanya maendeleo ya kiroho.

  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 45]

      Madalena

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki