Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Arusi Zenye Shangwe Zinazomletea Yehova Heshima
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Mei 1
    • Inaelekea kwamba kulikuwa na muziki ufaao na watu walicheza dansi kwa adabu kwa sababu ilikuwa kawaida kuwa na dansi katika vikusanyiko vya Wayahudi. Yesu alionyesha jambo hilo katika mfano wake maarufu wa mwana mpotevu. Baba tajiri katika hadithi hiyo alifurahi sana kuona mwana wake aliyetubu amerudi hivi kwamba alisema: “Acheni tule na kujifurahisha wenyewe.” Kulingana na Yesu, sherehe hiyo ilitia ndani “utumbuizo wa kimuziki na uchezaji-dansi.”—Luka 15:23, 25.

      Hata hivyo, ni jambo la kutokeza kwamba Biblia haitaji muziki wala kucheza dansi kwenye arusi ya Kana.

  • Arusi Zenye Shangwe Zinazomletea Yehova Heshima
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Mei 1
    • Katika arusi fulani za Wakristo huku Afrika, vyombo vyenye nguvu sana vya muziki hutumiwa. Muziki waweza kuwa wenye sauti kubwa sana hivi kwamba wageni hawawezi kuzungumza kwa starehe.

  • Arusi Zenye Shangwe Zinazomletea Yehova Heshima
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Mei 1
    • Isitoshe, mara nyingi muziki wenye sauti kubwa huwavutia watu wenye fujo ambao huja bila kualikwa.

      Kwa kuwa masimulizi ya Biblia ya arusi hayasisitizi muziki na dansi, je, jambo hilo halipasi kuwaongoza wale wanaopanga kufanya arusi ambayo itamletea Yehova heshima?

  • Arusi Zenye Shangwe Zinazomletea Yehova Heshima
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Mei 1
    • Na wakiamua kuwa na muziki, wanapaswa kuchagua muziki ufaao na msimamizi anayestahili ahakikishe muziki si wenye sauti kupita kiasi. Wageni hawapaswi kuanza kutawala na kuleta muziki wenye kutilika shaka au kuongeza sauti ya muziki kwa kiasi ambacho hakifai.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki