-
Walilipenda Neno la MunguMnara wa Mlinzi—2009 | Juni 1
-
-
Biblia Ndani ya Mto wa Kitanda
Majuma mawili baada ya kufunga ndoa mnamo Februari (Mwezi wa 2) 1812, mmishonari Mwamerika Adoniram Judson pamoja na mke wake, Ann, walisafiri kwa muda mrefu, na hatimaye wakaamua kuishi Burma mwaka wa 1813.a Bila kukawia walianza kujifunza Kiburma, ambayo ni moja kati ya lugha ngumu zaidi duniani. Baada ya kujifunza kwa miaka kadhaa, Judson aliandika: “Tunajifunza lugha inayozungumzwa na watu katika upande mwingine wa dunia, na mpangilio wa mawazo yao ni tofauti na wetu . . . Hatuna kamusi wala mtu wa kutusaidia kuelewa maana ya neno hata moja.”
Judson hakukatishwa tamaa na matatizo ya lugha. Alikamilisha tafsiri ya Maandiko ya Kikristo ya Kigiriki katika Kiburma mnamo Juni (Mwezi wa 6) 1823. Baadaye, Burma iliingia vitani. Judson alishukiwa kuwa mpelelezi, hivyo akatupwa gerezani, akafungwa pingu sita za chuma, na kufungiliwa kwenye ufito mrefu. Katika kitabu chake cha mwaka wa 1853, Francis Wayland, aliandika hivi kumhusu Judson: “Bwana Judson alipojua kwamba ameruhusiwa kukutana na mke wake na kuzungumza naye Kiingereza, alitaka kwanza kabisa kujua kuhusu hati ya Agano Jipya iliyokuwa imetafsiriwa.” Ann akihofia kuwa hati hiyo iliyokuwa imefichwa chini ya sakafu ndani ya nyumba inaweza kuharibiwa na unyevunyevu na kuvu, aliitia ndani ya mto wa kitanda na kuushona, kisha akampelekea mume wake gerezani. Licha ya hali hizo ngumu, hati hiyo haikuharibika.
Baada ya miezi mingi gerezani, Judson aliachiliwa. Lakini furaha yake ilikuwa ya muda tu. Baadaye mwaka huohuo, Ann aliugua homa kali, akafa majuma kadhaa baadaye. Miezi sita tu baada ya tukio hilo, binti yake, Maria, mwenye umri wa miaka miwili hivi akafa kwa ugonjwa usioweza kupona. Ingawa alivunjika moyo sana, Judson alirudia kazi yake. Hatimaye akaikamilisha Biblia nzima mwaka wa 1835.
-
-
Walilipenda Neno la MunguMnara wa Mlinzi—2009 | Juni 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 11]
Adoniram Judson na tafsiri yake ya Biblia ya Kiburma
[Hisani]
Judson: Engraving by John C. Buttre/Dictionary of American Portraits/Dover
-