Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tulikotumwa Kuwa Mishonari Kumekuwa Nyumbani
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Desemba 1
    • Tangu tulipowasili nchini, tulikuwa na hamu kubwa ya kueneza ujumbe wa Biblia kwa wenyeji wa makabila ya Ovambo, Herero, na Nama. Lakini haikuwa rahisi. Nyakati hizo, nchi ya Kusini-Magharibi ya Afrika ilikuwa chini ya utawala wa serikali ya Afrika Kusini iliyozingatia ubaguzi wa rangi. Hatukuruhusiwa kuhubiri kwenye makazi ya watu weusi bila kibali cha serikali kwa sababu tulikuwa wazungu. Tuliomba kibali mara kwa mara, lakini wenye mamlaka walikataa kutupatia.

  • Tulikotumwa Kuwa Mishonari Kumekuwa Nyumbani
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Desemba 1
    • Lakini juma lilelile ambalo tulipanga kuondoka, wenye mamlaka walinipa kibali cha kwenda kwenye eneo la watu weusi la Katutura. Sasa tungefanya nini? Je, tungerudisha kibali hicho baada ya kukitafuta kwa miaka saba? Ilikuwa rahisi kusema kwamba wengine wataendelea na kazi hiyo. Lakini je, hii haikuwa zawadi kutoka kwa Yehova na jibu kwa sala zetu?

      Nilifanya uamuzi mara moja. Ningebaki nchini, kwa sababu niliogopa kwamba ombi letu la kibali chetu cha uraia lingetupiliwa mbali kama tungeondoka sote na kurudi Australia. Siku iliyofuata, nilirudisha tiketi yangu ya kusafiri kwa meli, na nikawaruhusu Coralie na Charlotte waende Australia kwa likizo ndefu.

      Walipokuwa Australia, nilianza kuhubiri eneo la watu weusi. Watu wengi sana walipendezwa. Coralie na Charlotte waliporudi, watu kadhaa wa eneo hilo walikuwa wakihudhuria mikutano yetu.

      Wakati huo nilikuwa na gari zee nililotumia kuwapeleka mikutanoni watu wenye kupendezwa. Nilisafiri mara nne au tano hivi wakati wa kila mkutano, na nilibeba watu saba, wanane, au tisa. Mtu wa mwisho aliposhuka, Coralie alikuwa akiniuliza hivi kwa utani: “Ni wangapi waliobaki chini ya kiti?”

      Ili tuwe na matokeo zaidi katika kazi ya kuhubiri, tulihitaji vichapo katika lugha ya wenyeji. Kwa hiyo nilikuwa na pendeleo la pekee la kufanya mpango wa kutafsiriwa kwa trakti ya Uzima Katika Ulimwengu Mpya katika lugha nne za wenyeji: Kiherero, Kinama, Kindonga, na Kwanyama. Watu wenye elimu tuliokuwa tukijifunza nao Biblia ndio waliokuwa watafsiri, lakini nilifanya kazi nao ili kuhakikisha kwamba kila sentensi ilitafsiriwa kwa usahihi. Lugha ya Kinama haina maneno mengi. Kwa mfano, nilikuwa nikijaribu kueleza wazo hili: “Hapo mwanzo Adamu alikuwa mtu mkamilifu.” Mtafsiri alijikuna-kuna kichwani na kusema kwamba hangeweza kukumbuka neno “mkamilifu” katika lugha ya Kinama. Mwishowe alisema, “nimelipata.” “Hapo mwanzo Adamu alikuwa kama tunda la pichi lililoiva.”

      Tumefurahia Tulikotumwa

      Miaka 49 imepita tangu tulipowasili katika nchi hii, ambayo sasa inaitwa Namibia. Leo si lazima kuwa na kibali ili kuingia maeneo ya watu weusi. Namibia inatawaliwa na serikali mpya ambayo inafuata katiba isiyozingatia ubaguzi wa rangi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki