-
Jinsi ya Kukabiliana na Kuvunjika MoyoMnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
-
-
● Naomi aliomboleza hivi: “Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana. Mimi nalitoka hali nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?”—Ruthu 1:20, 21.
-
-
Jinsi ya Kukabiliana na Kuvunjika MoyoMnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 15
-
-
Naomi aliyefiwa hakuruhusu msiba kumzuia asishiriki na watu wengine huko Moabu baada ya kifo cha mume na wana wake wawili. Hata hivyo, yaelekea alikuwa na roho chungu kujihusu na kuhusiana na wake wawili wa wana wake. Alipowahimiza warudi kwao, Naomi alisema hivi: “Maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa BWANA umetoka juu yangu.” Alipowasili Bethlehemu, alisisitiza hivi tena: “Msiniite Naomi [“Kupendeza”], niiteni Mara [“Uchungu”], kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.”—Ruthu 1:13, 20.
Hata hivyo, Naomi hakujitenga na Yehova na watu wake kwa kuendelea kuomboleza kwa muda mrefu. Alipokuwa Moabu alikuwa amesikia kwamba “BWANA amewajilia watu wake na kuwapa chakula.” (Ruthu 1:6) Alielewa kwamba kuishi miongoni mwa watu wa Yehova kulikuwa kwema kwake. Baada ya hapo, Naomi alirejea Yuda pamoja na Ruthu, mke wa mwana wake na kumwelekeza Ruthu kwa busara jinsi alivyopaswa kutenda kuhusiana na mkombozi wake, Boazi.
Vivyo hivyo leo, watu waaminifu ambao wamefiwa na wenzi wao hukabili mikazo ya kihisia kwa mafanikio wakiwa na shughuli nyingi katika kutaniko la Kikristo. Kama vile Naomi, wao wanaendelea kuzingatia mambo ya kiroho kwa kusoma Neno la Mungu kila siku.
-