-
Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na mataifa yatatembea kwa njia ya nuru yalo, na wafalme wa dunia wataleta utukufu wao ndani yalo.
-
-
Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
16. Ni nani walio “mataifa” ambayo yatatembea kwa njia ya nuru ya Yerusalemu Jipya?
16 Ni nani walio “mataifa” haya yanayotembea kwa njia ya nuru ya Yerusalemu Jipya? Hao ni watu, waliokuwa wakati mmoja sehemu ya mataifa ya huu ulimwengu mbovu, ambao huitikia nuru inayotolewa kupitia jiji hili tukufu la kimbingu. Wa kwanza kabisa katika hao ni umati mkubwa, ambao tayari umetoka katika “mataifa yote na makabila na vikundi vya watu na ndimi” na ambao huabudu Mungu mchana na usiku wakiwa kampuni moja na jamii ya Yohana. (Ufunuo 7:9, 15, NW) Baada ya Yerusalemu Jipya kuja chini kutoka katika mbingu na Yesu kutumia funguo za kifo na za Hadesi kufufua wafu, wao wataungwa na mamilioni zaidi, ambao hapo awali walitoka katika “mataifa,” wanaokuja kumpenda Yehova na Mwana wake, Mume wa Yerusalemu Jipya aliye mithili ya Mwana-Kondoo.—Ufunuo 1:18.
-