-
Kufisha Babuloni MkubwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Na pembe kumi ambazo wewe uliona, na hayawani-mwitu, hizi zitachukia kahaba na zitafanya yeye kuwa mwenye kuteketezwa na mwenye uchi, na zitakula kabisa sehemu zake zenye mnofu na zitachoma yeye kabisa kabisa kwa moto.’”—Ufunuo 17:15, 16, NW.
16. Ni kwa nini Babuloni Mkubwa hataweza kutegemea maji yake yamuunge mkono wa himaya wakati serikali za kisiasa zinapomgeukia?
16 Kama vile Babuloni wa kale alivyotegemea ulinzi wa maji yake, Babuloni Mkubwa leo anategemea washiriki wake wengi mno “vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi.” Kwa kufaa malaika huelekeza uangalifu wetu kwenye hao kabla ya kusimulia tukio lenye kugutusha: Serikali za kisiasa za dunia hii zitamgeukia kijeuri Babuloni Mkubwa.
-
-
Kufisha Babuloni MkubwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
17. (a) Ni kwa sababu gani ukwasi wa Babuloni Mkubwa hautamwokoa? (b) Mwisho wa Babuloni Mkubwa utakuwaje wenye aibu kabisa? (c) Mbali na pembe kumi, au mataifa moja moja, ni nini kingine kinachojiunga katika jeuri dhidi ya Babuloni Mkubwa?
17 Kwa hakika, ukwasi mkubwa mno wa vitu vya kimwili hautaweza kumwokoa Babuloni Mkubwa. Huenda hata ukaharakisha kuharibiwa kwake, kwa kuwa njozi huonyesha kwamba wakati hayawani-mwitu na pembe kumi wanapomwonyesha chuki yao watamvua majoho yake ya kifalme na vito vyake vyote vya thamani. Wao watapora ukwasi wake. ‘Wanamfanya kuwa uchi,’ wakifichua kiaibu tabia yake halisi. Mteketezo wee! Pia mwisho wake ni wenye aibu kabisa. Wanamharibu, na ‘kula sehemu zake zenye mnofu,’ wakimwacha mifupa mitupu isiyo na uhai. Mwishowe, wao ‘humchoma kabisa kabisa kwa moto.’ Yeye huchomwa kabisa kama mwenye ugonjwa wa tauni, bila hata maziko ya heshima! Si mataifa yale tu, kama yanavyowakilishwa na pembe kumi, yanayomharibu kahaba mkubwa, bali pia “hayawani-mwitu,” kumaanisha UM wenyewe, hujiunga nayo katika kuonyesha jeuri hii. Utatoa idhini yao ili dini bandia iharibiwe. Yaliyo mengi ya yale mataifa 190 na zaidi yaliyo ndani ya UM yameonyesha tayari, kwa kiolezo chayo cha kupiga kura, uhasama wayo kuelekea dini, hasa ile ya Jumuiya ya Wakristo.
18. (a) Ni uwezekano gani wa mataifa kugeukia dini za Kibabuloni ambao tayari umeonekana? (b) Ni nini itakayokuwa sababu ya msingi ya shambulio la ujumla juu ya kahaba mkubwa?
18 Ni kwa nini hayo yangemtenda kijeuri hivyo hawara wao wa zamani? Sisi tumeona katika historia ya hivi majuzi uwezekano kama huo wa kugeukia dini ya Kibabuloni. Upinzani rasmi wa kiserikali umepunguza sana uvutano wa dini katika nchi kama vile China na nchi zilizokuwa Muungano wa Sovieti. Katika maeneo ya Kiprotestanti ya Ulaya, ubaridi wenye kuenea pote na mashaka vimeyaacha makanisa yakiwa tupu, hivi kwamba karibu dini imekufa. Milki kubwa mno ya Kikatoliki imegawanywa na uasi na kutoafikiana ambavyo viongozi wake wameshindwa kutuliza. Ingawa hivyo, haitupasi kupoteza mwono wa uhakika wa kwamba hili shambulio la mwisho kabisa, la ujumla juu ya Babuloni Mkubwa linakuja likiwa wonyesho wa hukumu ya Mungu isiyobadilika juu ya kahaba mkubwa.
Kufikiliza Fikira ya Mungu
19. (a) Utekelezo wa hukumu ya Yehova dhidi ya kahaba mkubwa unaweza kutolewaje kielezi na hukumu yake dhidi ya Yerusalemu asi-imani katika 607 K.W.K.? (b) Hali ya ukiwa, ya kutokaliwa ya Yerusalemu baada ya 607 K.W.K. ilitangulia kutoa tamathali ya nini kwa siku yetu?
19 Yehova anatekelezaje hukumu hii? Hii inaweza kutolewa kielezi na tendo la Yehova dhidi ya watu wake waasi-imani katika nyakati za kale, ambao kuwahusu yeye alisema: “Katika manabii wa Yerusalemu mimi nimeona vitu vibaya sana, kufanya uzinzi na kutembea katika ubandia; na wao wameimarisha mikono ya watenda maovu ili kwamba isiwapase kurudi, kila mmoja kutoka ubaya wake mwenyewe. Kwangu mimi wao wote wamekuwa kama Sodoma, na wakaaji wake ni kama Gomora.” (Yeremia 23:14, NW) Katika 607 K.W.K., Yehova alitumia Nebukadneza ‘avue mavazi, atwae vitu vizuri, na aache uchi na bila nguo’ jiji hilo lenye uzinzi wa kiroho. (Ezekieli 23:4, 26, 29, NW) Yerusalemu la wakati huo lilikuwa kigezo cha Jumuiya ya Wakristo ya leo, na kama alivyoona Yohana katika njozi ya mapema zaidi, Yehova ataipa Jumuiya ya Wakristo na dini nyingine yote bandia adhabu inayofanana na hiyo. Ukiwa, hali ya kutokaliwa ya Yerusalemu baada ya 607 K.W.K. huonyesha vile Jumuiya ya Wakristo ya kidini itakavyoonekana baada ya kuvuliwa ukwasi wayo na kufichuliwa kiaibu. Na sehemu inayobaki ya Babuloni Mkubwa haitakuwa afadhali.
20. (a) Yohana anaonyeshaje kwamba kwa mara nyingine tena Yehova atatumia watawala wa kibinadamu kutekeleza hukumu? (b) “Fikira” ya Mungu ni nini? (c) Ni katika njia gani mataifa yatafikiliza “fikira moja,” yayo lakini kwa kweli ni fikira ya nani itatimizwa?
20 Kwa mara nyingine tena Yehova anatumia watawala wa kibinadamu kutekeleza hukumu. “Kwa maana Mungu alitia hilo ndani ya mioyo yao kufikiliza fikira yake, hata kufikiliza fikira yao moja kwa kumpa ufalme wao hayawani-mwitu, mpaka hapo maneno ya Mungu yatakuwa yametimilizwa.” (Ufunuo 17:17, NW) “Fikira” ya Mungu ni nini? Kupangia wafishaji wa Babuloni Mkubwa waungane pamoja, ili kumharibu kabisa. Bila shaka, matilaba ya watawala katika kumshambulia yatakuwa kufikiliza “fikira moja” yao wenyewe. Wao watahisi kwamba ni kwa masilahi yao ya utukuzaji wa taifa kumgeukia huyo kahaba mkubwa. Huenda wakaja kuona kule kuendelea kwa dini iliyopangwa kitengenezo ndani ya mipaka yao kuwa tisho kwa enzi zao. Lakini Yehova atakuwa kwa kweli akiongoza mambo kwa werevu; wao watafikiliza fikira yake kwa kuharibu kwa dharuba moja adui yake mzinzi wa muda mrefu!—Linga Yeremia 7:8-11, 34.
21. Kwa kuwa hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu atatumiwa katika kuharibu Babuloni Mkubwa, kwa wazi mataifa yatafanya nini kwa habari ya Umoja wa Mataifa?
21 Ndiyo, mataifa yatatumia hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, Umoja wa Mataifa, katika kuharibu Babuloni Mkubwa. Wao hawatendi kwa utangulizi wao wenyewe, kwa maana Yehova hutia ndani ya mioyo yao “hata kufikiliza fikira moja yao kwa kumpa ufalme wao hayawani-mwitu.” Wakati ujapo, kwa wazi mataifa yataona uhitaji wa kuimarisha Umoja wa Mataifa. Itakuwa kana kwamba, wanaupa meno, wakiupa mamlaka yoyote na nguvu waliyo nayo ili kwamba uweze kugeukia dini bandia na kupiga vita kwa kufaulu dhidi yayo “mpaka hapo maneno ya Mungu yatakuwa yametimilizwa.” Hivyo, kahaba wa kale atakuja kwenye mwisho wake kabisa. Na apotelee mbali!
-