Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Nepal

      Purnamaya mwenye umri wa miaka 16 anaishi kwenye mji mdogo huko Nepal. Mjomba wake alimhubiria na akaanza kujifunza. Sasa, yeye anahudhuria mikutano mara moja kwa juma bila kukosa, ingawa anahitaji kusafiri kwa basi muda wa saa mbili na nusu ili kufika kutanikoni. Si rahisi kwake kufanya hivyo. Wazazi wake wana ukoma, kwa hiyo wao ni maskini sana. Asubuhi na mapema, Purnamaya anavunja mawe kutengeneza kokoto ili kuitegemeza familia yao kifedha, mbali na kufanya kazi za nyumbani kama kupika na kufua nguo. Isitoshe, yeye anaenda shuleni. Ili kufika kwenye mikutano, Purnamaya analipa nauli inayolingana na mshahara ambao mfanyakazi analipwa kwa siku moja. Nyakati nyingine, wazazi wake wanamtia moyo aende katika kanisa lililo karibu. Lakini Purnamaya anajua kwamba anaweza kujifunza kumhusu Yehova katika Jumba la Ufalme tu, kwa hiyo anajitahidi kuhudhuria mikutano. Hivi karibuni, ilimbidi auze saa yake aliyopewa na nyanyake kama zawadi. Yeye anatoa maelezo mazuri mikutanoni na pia anawaeleza watu katika mji wao mambo anayojifunza. Anawatia moyo watu wote wanaomjua.

  • Kuhubiri na Kufundisha Duniani Kote
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 53]

      Purnamaya akitengeneza kokoto ili kuitegemeza familia yao

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki