-
‘Nafsi Zilizochinjwa’ ZathawabishwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Likiripoti juu ya Hitla kunyanyasa Mashahidi wa Yehova, pitio la kitabu Kirchenkampf in Deutschland (Vita ya Makanisa Katika Ujeremani) lilitaarifu hivi: “Theluthi moja yao [Mashahidi] waliuawa, ama walifishwa kwa amri ya kiserikali, ama kwa matendo mengine ya jeuri, njaa, ugonjwa au kazi ngumu ya utumwa. Ukali wa utiisho huu ulikuwa bila kitangulizi na ulikuwa tokeo la imani thabiti ambayo haingeweza kupatanishwa na siasa ya Usoshalisti wa Kitaifa.”
-
-
‘Nafsi Zilizochinjwa’ ZathawabishwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
10. Wanaume vijana wa ule umati mkubwa wamepatwa na minyanyaso gani katika mabara mengi?
10 Tangu 1935 wanaume vijana waaminifu wa ule umati mkubwa wamehimili ukali wa minyanyaso katika mabara mengi. (Ufunuo 7:9) Hata wakati Vita ya Ulimwengu 2 ilipokuwa ikiisha katika Ulaya, katika mji mmoja tu vijana Mashahidi wa Yehova 14 walifishwa kwa kunyongwa kwa amri ya kiserikali. Uhalifu wao? Kukataa ‘kujifunza vita tena.’ (Isaya 2:4) Karibuni zaidi, wanaume vijana katika Mashariki na katika Afrika wamepigwa mpaka kifo au wakauawa na kikosi cha wapiga risasi kwa amri ya kiserikali juu ya suala ilo hilo. Wafia-imani hawa vijana, wategemezaji wastahilifu wa ndugu za Yesu wapakwa-mafuta, hakika watapata ufufuo kuingia ndani ya ile dunia mpya iliyoahidiwa.—2 Petro 3:13; Linga Zaburi 110:3; Mathayo 25:34-40; Luka 20:37, 38.
-