Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Hakutuacha Kamwe
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
    • Kutahiniwa Juu ya Suala la Kutokuwamo

      Ingawa vita iliisha 1945, magumu yetu yaliendelea nayo hata yakawa mabaya zaidi. Kupiga kura kwa lazima kulitekelezwa wakati wa uchaguzi wa Desemba 2, 1946. Yeyote yule aliyethubutu kutopiga kura alionwa kuwa adui wa Serikali. Wale wa kutaniko letu katika Përmet wakaanza kuuliza, “Twapaswa tufanyeje?”

      “Ikiwa mwamtumainia Yehova,” nikajibu, “hampaswi kuniuliza jambo la kufanya. Tayari mwajua kwamba watu wa Yehova hawaungi mkono upande wowote. Wao si sehemu ya ulimwengu.”—Yohana 17:16.

      Siku ya uchaguzi ikaja, na wajumbe wa serikali wakaja nyumbani kwetu. Wakaanza hivi kwa utulivu, “Ah, acheni tunywe kikombe cha kahawa na kuongea. Je, wajua leo ni siku gani?”

      “Ndiyo, uchaguzi unafanywa leo,” nikajibu.

      “Ni afadhali uharakishe, au utachelewa,” ofisa mmoja akasema.

      “La, sina nia ya kwenda. Kura yetu ni kwa Yehova,” nikajibu.

      “Haya basi, njoo upigie kura upinzani.”

      Nikaeleza kwamba Mashahidi wa Yehova hawaungi mkono upande wowote kabisa. Msimamo wetu ulipojulikana na wengi, tuliwekewa mkazo zaidi. Tuliamuriwa tuache kufanya mikutano yetu, kwa hiyo tukaanza kukutana kwa siri.

  • Yehova Hakutuacha Kamwe
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
    • Lakini kutokuwamo kwetu kuliongoza kwenye kuondoshwa kwa majina yetu katika orodha za wale wa kupewa chakula. Kwa hiyo, maisha yalikuwa magumu sana.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki