-
Sehemu ya 4—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Wenzi wengine wa ndoa, John na Ellen Hubler, walienda New Caledonia kuanzisha kazi huko. Walipowasili katika 1954, walikuwa na visa za watalii za mwezi mmoja tu. Lakini John alipata kazi ya kimwili, nalo hilo likawasaidia kupata kuongezewa muda. Baada ya wakati, Mashahidi wengine—jumla ya 31—wakahamia humo kwa njia iyo hiyo. Mwanzoni, walikuwa wakifanya huduma yao katika maeneo ya viungani ili wasivute fikira sana. Baadaye, walianza kuhubiri katika jiji kuu, Nouméa. Kutaniko likaundwa. Kisha, katika 1959, mshiriki wa Aksio ya Katoliki akapata cheo kikubwa serikalini. Visa za Mashahidi hazikufanywa upya tena. Akina Hubler wakalazimika kuondoka. Vichapo vya Watch Tower vikapigwa marufuku.
-
-
Sehemu ya 4—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Picha katika ukurasa wa 471]
John na Ellen Hubler, wakifuatwa na Mashahidi wengine 31, walihamia New Caledonia. Kabla ya kulazimika kuondoka, kutaniko lilikuwa limesimamishwa imara huko
-