Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kondoo Wengine na Agano Jipya
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Februari 1
    • “Agano Lidumulo Milele”

      13, 14. Ni katika njia zipi agano jipya ni lenye kudumu milele?

      13 Ni nini kitukiacho wale wa mwisho wa 144,000 wapatapo utimizo wa tumaini lao la kimbingu? Je, agano jipya litakoma kutumika? Wakati huo hakutakuwa mshiriki yeyote wa Israeli wa Mungu mwenye kubaki duniani. Washiriki wote katika hilo agano watakuwa pamoja na Yesu “katika ufalme wa Baba [yake].” (Mathayo 26:29) Lakini twakumbuka maneno haya ya Paulo katika barua yake kwa Waebrania: ‘Mungu wa amani alimleta kutoka kwa wafu mchungaji mkubwa wa kondoo kwa damu ya agano lidumulo milele.’ (Waebrania 13:20; Isaya 55:3) Ni katika maana gani agano jipya ni lenye kudumu milele?

      14 Kwanza, tofauti na agano la Sheria, hakuna jingine litakalochukua mahali pake. Pili, matokeo ya utendaji-kazi wake ni yenye kudumu, kama vile umaliki wa Yesu ulivyo. (Linganisha Luka 1:33 na 1 Wakorintho 15:27, 28.) Ufalme wa kimbingu una mahali pa milele katika makusudi ya Yehova. (Ufunuo 22:5) Na tatu, kondoo wengine wataendelea kunufaika na mpango wa agano jipya. Wakati wa Utawala wa Miaka Elfu wa Kristo, wanadamu waaminifu watafuliza ‘kumtolea Yehova utumishi mtakatifu mchana na usiku katika hekalu lake’ kama vile wafanyavyo sasa.

  • Kondoo Wengine na Agano Jipya
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Februari 1
    • 17. Kila mmoja wetu apaswa aazimie kufanya nini kwa kufikiria shangwe itungojeayo?

      17 “Agano lidumulo milele” litatimiza fungu jipi, ikiwa kuna fungu lolote, katika muhula wenye kusisimua utakaoanza wakati huo? Hatuwezi kusema juu ya hilo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki