Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Kukanyagwa kwa Ua

      7. (a) Ni kwa nini Yohana anaambiwa asipime ua? (b) Ni wakati gani jiji takatifu lilipokanyagwa chini ya nyayo kwa miezi 42? (c) Viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walishindwaje kutegemeza viwango vya uadilifu vya Yehova kwa miezi 42?

      7 Ni kwa nini Yohana alikatazwa kupima ua? Yeye anatuambia kwa maneno haya: “Lakini kwa habari ya ua ambao uko nje ya patakatifu pa hekalu, utupe nje kabisa na usiupime, kwa sababu umepewa kwa mataifa, na wao watakanyaga jiji takatifu kwa miezi arobaini na miwili.” (Ufunuo 11:2, NW) Tumeona kwamba ua wa ndani ni picha ya msimamo wa uadilifu duniani wa Wakristo waliozaliwa kwa roho. Kama tutakavyoona, rejezo hapa ni kwa miezi 42 halisi iliyoendelea kuanzia Desemba 1914 mpaka Juni 1918, wakati wote wadaio kuwa Wakristo walitiwa katika mtihani mkali. Je! wao wangeshikilia viwango vya uadilifu vya Yehova katika pindi ya hiyo miaka ya vita? Walio wengi hawakufanya hivyo. Kwa ujumla, viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo waliweka utukuzo wa taifa mbele ya kutii sheria ya kimungu. Katika pande zote mbili za vita hiyo, ambayo ilipiganwa hasa katika Jumuiya ya Wakristo, viongozi wa kidini waliwahubiri vijana waingie katika mahandaki ya vita. Mamilioni kadhaa walichinjwa. Kufikia wakati hukumu ilianza na nyumba ya Mungu katika 1918, United States ilikuwa pia imeingia katika umwagaji-damu huo, na viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo yote walikuwa wamejitia katika hatia ya damu ambayo ingali inapiga kilio kwa ajili ya kisasi cha kimungu. (1 Petro 4:17) Kutupwa nje kwao kumekuwa kwa kudumu, kusikobadilika.—Isaya 59:1-3, 7, 8; Yeremia 19:3, 4.

      8. Wakati wa Vita ya Ulimwengu 1, wengi wa Wanafunzi wa Biblia walikuja kung’amua nini, lakini ni jambo gani ambalo hawakuthamini kikamili?

      8 Ingawa hivyo, vipi kikundi kidogo cha Wanafunzi wa Biblia? Je! wangepimwa mara hiyo katika 1914 kwa kushikamana kwao na viwango vya kimungu? La. Kama vile wale wanaodai kuwa Wakristo katika Jumuiya ya Wakristo, wao vilevile lazima watahiniwe. ‘Walitupwa nje kabisa, wakapewa kwa mataifa’ wajaribiwe vikali na kunyanyaswa. Wengi wao waling’amua kwamba hawapaswi kwenda nje wakaue binadamu mwenzao, lakini bado hawakuwa wamethamini kikamili kutokuwamo kwa Kikristo. (Mika 4:3; Yohana 17:14, 16; 1 Yohana 3:15) Chini ya mkazo kutoka mataifa, baadhi yao waliacha msimamo wao.

      9. Ni jiji takatifu gani ambalo lilikanyagwa chini ya nyayo na mataifa, na duniani, ni nani waliowakilisha jiji hilo?

      9 Ingawa hivyo, ni jinsi gani jiji takatifu lilikanyagwa na mataifa hayo? Kwa wazi, hii hairejezei Yerusalemu lililoharibiwa zaidi ya miaka 25 kabla Ufunuo haujaandikwa. Badala ya hivyo, hilo jiji takatifu ni Yerusalemu Jipya, linaloelezwa baadaye katika Ufunuo, ambalo linawakilishwa duniani sasa na mabaki ya Wakristo wapakwa-mafuta walio katika ua wa ndani wa hekalu. Baada ya wakati kupita, hawa pia watakuwa sehemu ya hilo jiji takatifu. Kwa hiyo kuwakanyaga ni sawasawa na kukanyaga hilo jiji takatifu lenyewe.—Ufunuo 21:2, 9-21.

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 12. Ni kwa nini kipindi cha wakati ambacho jiji takatifu lingekanyagwa chini ya nyayo huonekana kuwa halisi?

      12 Jamii ya Yohana ilipaswa ihubiri ujumbe huu kwa wakati dhahiri uliotajwa: siku 1,260, au miezi 42, urefu ule ule wa wakati ambao jiji takatifu lingekanyagwa chini ya nyayo. Kipindi hiki kinaonekana kuwa halisi, kwa maana kinasemwa kwa njia mbili tofauti, kwanza kwa miezi na kisha kwa siku. Kwa kuongezea, mwanzoni mwa siku ya Bwana, kulikuwako wakati uliotiwa alama wa miaka mitatu na nusu ambao magumu yaliyowapata watu wa Mungu yalilingana na matukio yaliyotolewa unabii hapa—kuanzia Desemba 1914 na kuendelea mpaka Juni 1918. (Ufunuo 1:10)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki